Monday, June 6, 2016

TSHABALALA AAMUA KUBADILI JINA MSIMU UJAO.




BEKI wa Simba na Taifa Stars, Mohamed Hussein 'Tshabalala' ametangaza rasmi kulikacha jina hilo la mchezaji wa zamani wa Afrika Kusini, Lawrence Siphiwe Tshabalala na kuanzia sasa atatumia jina la ZIMBWE Jr.

Beki huyo ambaye katika mchezo wa jana dhidi ya Misri aligeuka kuwa nyota baada ya kuingia dakika za mwisho, Amesema kuwa ametafakari sana juu ya matumizi ya jina la Tshabalala na kugundua kuwa anafanya makosa.


"Sioni faida ya kuendelea kulitumia jina  ambalo si langu, hainifurahishi ninavyosikia watu wakiniita Tshabalala wakati hata sina undugu na huyo mtu," alisema Zimbwe Jr


Beki huyo alifafanua kuwa ameona ni bora aanze kutumia jina la mjomba wake Said Zimbwe Mwaibambe ambaye kwasasa ni marehemu. Zimbwe aliwahi kuichezea Yanga ya jijini Dar es Salaam enzi za uhai wake.


Akielezea chanzo cha jina hilo, Zimbwe Jr alisema "Nilikuwa natazama mechi moja ya timu ya Taifa ya Afrika Kusini  nikamuona jamaa akicheza ndipo nilipovutiwa na uchezaji wake. 


"Kiukweli nilitamani sana kucheza kama yeye, kwahiyo nilipotoka pale nikaenda kuandika hilo jina la Tshabalala kwenye jezi ya timu yangu ya zamani Bom Bom FC, kuanzia hapo ndio nikawa naitwa hivyo," alisema Zimbwe Jr


Zimbwe Jr ameviomba vyombo vya habari na wadau wa soka kwa ujumla wamsaidie katika kufanikisha azma yake hiyo ya kufahamika kwa jina hilo jipya badala ya Tshabalala lililokaa sana midomoni mwa  watu.

0 Responses to “TSHABALALA AAMUA KUBADILI JINA MSIMU UJAO.”

Post a Comment

More to Read