Sunday, June 5, 2016

RAIS WA ANGOLA AMTEUA BINTI YAKE AMABAYE NI MWANAMKE TAJIRI AFRIKA KUWAB MKUU WA SHIRIKA LA MAFUTA LA SERIKALI





Rais wa Angola anazidi kuhakikisha kuwa mashavu yanayotokana na utajiri mkubwa wa mafuta na gesi wa nchi yake yanabaki ndani ya familia.

Rais Jose Eduardo dos Santos amemteua binti yake, Isabel kuwa mkuu wa shirika la mafuta linalomilikiwa na serikali, Sonangol.
Angola, kumiliki visima vya mafuta ni sawa na kuitawala nchi. 

Uteuzi huo wa binti yake ni dalili za kutaka kutafuta maboresho kwenye sekta hiyo ya mafuta inayododa nchini humo. Lakini wakosoaji wanadai hakuna lolote bali ni janja ya rais huyo anayetuhumiwa kwa ufisadi mkubwa kuvuna utajiri zaidi.

Dos Santos ambaye amekuwa madarakani kwa miaka 36, ni rais wa pili Afrika aliyekaa madarakani kwa muda mrefu zaidi. Ameahidi kuachia madaraka mwaka 2018.

Isabel dos Santos, 43, ana utajiri wa dola bilioni 3.3 ambao unahusishwa na mali za serikali.
Mali zake ni pamoja na kumiliki asilimia 25 ya shirika la mawasiliano ya simu Angola, Unitel. Pia anamiliki asilimia 7 ya shirika la mafuta la Ureno, Galp Energia, hisa kwenye kampuni ya runinga ya Ureno pamoja na hisa nyingi kwenye moja ya benki kubwa za Angola, Banco BIC na mwingine. Hisa zake 18.6% kwenye benki ya pili kwa ukubwa Ureno, BPI zinauzwa. Isabel dos Santos pia anamiliki maduka kibao na klabu ya usiku.

Sonangol inasimamia hazina kubwa ya mafuta na gesi nchini Angola na inachangia nusu ya pato la taifa.
Wakati huo huo kaka zake, Welwitchea José dos Santos na José Paulino dos Santos wanamiliki Semba, kampuni ya mawasiliano ambayo hupewa tenda za serikali katika miradi ya masoko na matangazo.

Semba imekuwa ikituhumiwa kwa kupokea fedha moja kwa moja kutoka kwenye bajeti ya serikali.

0 Responses to “RAIS WA ANGOLA AMTEUA BINTI YAKE AMABAYE NI MWANAMKE TAJIRI AFRIKA KUWAB MKUU WA SHIRIKA LA MAFUTA LA SERIKALI”

Post a Comment

More to Read