Friday, July 15, 2016
TRA YAKABIDHI EFDS 130 KWA MAKATIBU WAKUU WA WIZARA ZOTE NCHINI.
Do you like this story?
MAMLAKA
ya Mapato Tanzania (TRA) imetoa mashine 130 za kielektroniki za kutoa
risiti (EFDs) kwa Makatibu Wakuu 25 wa wizara zote nchini kwa ajili ya
taasisi na mamlaka zao, zenye wajibu wa kukusanya mapato ya serikali ili
kuhakikisha wanaokoa mapato ya serikali yanayopotea.
Akizungumza
jana Dar es Salaam wakati wa kukabidhi mashine hizo, Kamishna Mkuu wa
TRA, Alphayo Kidata alisema kila wizara itapewa mashine tano ili
kuboresha ukusanyaji wa mapato.
“Kila
Katibu Mkuu tunamkabidhi mashine tano za EFDs zitakazosaidia
kuhakikisha serikali inapata mapato yake na hivyo kuokoa mapato ya
serikali ambayo yanapotea,” alisema na kuongeza:
“Tunatarajia
mashine hizi zitatumika mahususi kutolea risiti, hivyo watumishi wote
wa serikali ambao wanafanya marejesho ya matumizi mbalimbali wanatakiwa
kuambatanisha risiti za mashine za EFDs”.
Aidha
alisema TRA inaendelea kudhibiti wafanyabiashara wanaokwepa kutumia
mashine za kielektroniki za kodi kwa kuwakamata na kuwatoza faini au
kuwafikisha mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria.
“Lengo
letu ni kuhakikisha tunafikia na kuvuka lengo la kukusanya Sh trilioni
15.5 kwa mwaka wa fedha 2016/2017 ambao tayari tumeuanza,” alisema.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “TRA YAKABIDHI EFDS 130 KWA MAKATIBU WAKUU WA WIZARA ZOTE NCHINI.”
Post a Comment