Friday, September 16, 2016
KUTOKA MAHAKAMANI: ZOMBE AACHIWA HURU, MWENZAKE AHUKUMIWA KUNYONGWA HADI KUFA
Do you like this story?
Mahakama
ya Rufani imemhukumu kunyongwa hadi kufa aliyekuwa Mkuu wa upelelezi wilaya ya
Kinondoni (OC-CID), Mrakibu wa Polisi (SP) Christopher Bageni, baada ya kumtia
hatiani kwa kosa ka mauaji ya wafanyabiashara watatu wa madini kutoka Mahenge
mkoani Morogoro.
Wakati
Bageni akihukumiwa kitanzi, aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi mkoa wa Dar (RCO),
Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Abdallah Zombe na maafisa wengine wawili wa
Polisi, Ahmed Makelle na Rajabu Bakari wameachiwa huru, baada ya mahakama
kuwaona kuwa hawana hatia.
Bageni
amehukumiwa adhabu hiyo leo baada ya mahakama ya Rufani kukubaliana na rufaa ya
Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP).
DPP
alikata rufaa akipinga hukumu ya Mahakama Kuu kuwaachia huru katika kesi ya
mauaji ya wafanyabiashara hao.
Wafanyabiashara
hao, Savings Chigumbi, Ephraim Chigumbi, Mathias Lunkombe na dereva teksi wa
Manzese, Juma Ndugu, waliuawa Januari 14,2006, kwa kupigwa risasi Mbezi Luis,
Dar.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “KUTOKA MAHAKAMANI: ZOMBE AACHIWA HURU, MWENZAKE AHUKUMIWA KUNYONGWA HADI KUFA”
Post a Comment