Friday, September 16, 2016
TAARIFA MUHIMU KUELEKEA MCHEZO WA EPL KATI YA CHELSEA NA LIVERPOOL
Do you like this story?
Ligi
Kuu ya England inaendelea leo ambapo Chelsea watakuwa nyumbani Stamford Bridge
kuwakaribisha Liverpool, mchezo utaofanyika saa 4:00 usiku kwa majira ya Afrika
Mashariki.
Taarifa
muhimu kutoka kila timu
Chelsea
David
Luiz atakuwa akicheza kwa mara ya kwanza tangu arejee klabuni hapo kutoka PSG
aliposajiliwa kwa ada ya paundi mil 34.
Luiz
atapangwa mahsusi kuziba pengo la nahodha na beki mkongwe wa klabu hiyo John
Terry, ambaye anasumbuliwa na maumivu ya kifundo cha mguu aliyopata katika
mchezo dhidi ya Swansea wikiendi iliyopita
Liverpool.
Beki
waa Liverpool Dejan Lovren anatarajiwa kurejea kikosini baada ya kukosekana
kwenye mchezo dhidi ya Leicester kutokana na kusumbuliwa na macho, ambapo
Liverpool walishinda mabao 4-1 win.
Philippe
Coutinho atajumuishwa kikosini leo baada ya kukosa mchezo uliopita kutokana na
kupumzishwa kufuatia safari ndefu kutoka Brazil.
Kauli
za mameneja
Kocha
wa Chelsea Antonio Conte: "David Luiz atacheza kwa mara ya kwanza na tunaamini
atafanya vizuri.
"Tunataraji
atacheza vizuri, na kwa umakini mkubwa. Sote tunafahamu kwamba David ni
mchezaji mzuri na tunajitahidi kwa hali na mali kuhakikisha anakuwa katika hali
nzuri ili kucheza katika kiwango bora.
"Nina
imani naye kubwa sana. Ni mchezaji mzuri na nimeona mambo mazuri sana wakati
akiwa mazoezini ."
Meneja
wa Liverpool Jurgen Klopp juu ya Diego Costa: "Ni mpambanaji wa ukweli
akiwa uwanjani. Anautumia mwili wake kisawasawa na huo ndio ubora wake. Kwenye
mchezo dhidi ya Swansea alionesha ubora wa hali ya juu.
"Ni
mchezaji wa kiwango cha dunia na hicho ndicho mashabiki wa soka wanaweza
kuongea juu ya Costa.
"Msimu
uliopita haukuwa mzuri kwa Chelsea na sasa wamerudi kwenye mstari, hivyo
tunahitaji kuwa makini kwelikweli."
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “TAARIFA MUHIMU KUELEKEA MCHEZO WA EPL KATI YA CHELSEA NA LIVERPOOL”
Post a Comment