Tuesday, October 18, 2016
BASI LA BARCELONA LAPATA AJALI NA KUUA WATU 10 MKOANI LINDI
Do you like this story?
Watu
10 wamefariki dunia na wengine 44 wamejeruhiwa baada ya basi la kampuni ya
Barcelona walilokuwa wakisafiria kutoka jijini Dar es Salaam kwenda mkoani
Lindi kupata ajali eneo na Miteja mkoani Lindi.
Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, Renata Mzinga imesema kuwa chanzo cha ajali hiyo kimetokana na tairi ya gari ya upande wa kushoto kupasuka na kutokana na mwendo wa kasi wa basi hilo, dereva alipoteza uelekeo ndipo likapinduka.
Pia
Kamanda Mzinga amesema kuwa wamechunguza na kugundua kua licha ya kuwa basi
hilo lilikuwa na uwezo wa kubeba abiria 48, wakati basi hilo linapata ajali
kulikuwa na abiria 54 kitu ambacho ni kosa kisheria.
Aidha,
Kamanda Mzinga amesema kuwa bado wanaendelea na uchunguzi kuweza kubaini alipo
dereva ili kuweza kufahamu ni kipi hasa kilichotokea. Hadi sasa wanamshikilia
kondakta wa basi hilo lakini bado hajaweza kuelezea tukio halisi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ BASI LA BARCELONA LAPATA AJALI NA KUUA WATU 10 MKOANI LINDI”
Post a Comment