Wednesday, October 12, 2016
SIMBA WAENDELEA KUKAA JUU MARA BAADA YA KUMNYUKA MBEYA CITY 2-0
Do you like this story?
Kikosi cha Simba |
Kikosi cha Mbeya City |
Wachezaji wa Simba wakimpongeza Ibrahim Ajibu aliefunga goli.(Picha na David Nyembe wa Fahari News Mbeya) |
Mashabiki wa Simba |
Kichuya akishangilia goli lake. |
Mashabiki wa Mbeya City |
Wekundu
wa Msimbazi Simba SC wakiwa jijini Mbeya kwenye Uwanja wa Sokoine kucheza na
wenyeji wao Mbeya City wameendeleza wimbi la ushindi baada ya kuibuka na
ushindi wa mabao 2-0.
Simba
walionekana kuwa na dalili za kuibuka na ushindi mapema tu baada ya washambulizi
wake Ibrahim Ajibu, Shiza Kichuya na Fredrick Blagnon kulisakama lango la Mbeya
City mithili ya nyuki.
Iliwachukua
dakika sita tu tangu filimbi ya mwamuzi ipulizwe Simba kupata bao kupitia kwa
Ibrahim Ajibu 'Fundi', ambaye alipiga mpira wa adhabu mujarab na kutinga moja
kwa moja wavuni,
Ajibu
aliendelea tena kulikasakama lango la Mbeya City baada ya kuachia shuti kali
dakika ya 15 lakini mpira uligonga mwamba na kurudi uwanjani kabla ya kuokolewa
na walinzi wa Mbeya City.
Simba
walipata penati baada ya Blagnon kufanyiwa madhambi na kupiga mwenyewe lakini
alikosa baada ya kipa wa Mbeya City kupangu mpira.
Kiungo
mshambuliaji wa pembeni wa Simba aliye kwenye kiwango bora kwa sasa, Shiza
Kichuya alifunga bao la pili mnamo dakika ya 33 baada ya kumhadaa beki wa Mbeya
City na kuupiga mpira kwa ufundi wa hali ya juu ya kuandika bao lake la sita
msimu huu akiwa ndio kinara wa mabao.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “SIMBA WAENDELEA KUKAA JUU MARA BAADA YA KUMNYUKA MBEYA CITY 2-0”
Post a Comment