Sunday, October 23, 2016
MAJAMBAZI MENGINE YAUAWA KATIKA MAPAMBANO MAKALI MKURANGA
Do you like this story?
Jeshi
la Polisi Mkoa wa Temeke limeua watu wanne wanaodhaniwa kuwa ni majambazi
katika wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani.
Akizungumza
na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa
Kipolisi Temeke, Gilles Muroto alisema tukio hilo ni la Oktoba 21 baada ya
polisi kupata taarifa za kuwepo kwa kundi la watu wanaodhaniwa ni majambazi.
Alisema
baada ya taarifa, kikosi kazi cha Polisi cha Kanda Maalumu ya Dar es Salaam,
kilifanya ufuatiliaji na kubaini nyumba ambayo haijakamilika imezungushiwa uzio
na muda wote mlango wa uzio huo ulikuwa umefungwa.
Aliongeza
kuwa uchunguzi wa kina, ulifanyika na kubaini kuwa kweli kundi hilo, lipo ndani
ya nyumba hiyo na kwamba muda mwingi mlango wa uzio, hufungwa na kuongeza kuwa
majira ya saa tano askari wa kikosi kazi cha mkoa huo na mkoa wa Pwani,
kilizingira nyumba hiyo.
“Baada
ya kujipanga mlango wa uzio huo uligongwa na kutoa amri ya kuwataka walioko
ndani ya nyumba hiyo wafungue mlango na kujisalimisha, lakini tulishangaa baada
ya amri hiyo ghafla milio ya risasi ilianza kutoka ndani ya nyumba hiyo,” alisema Muroto.
Aliongeza
kuwa baada ya milio hiyo, askari ambao walikuwa makini na wakiwa wamezingira
nyumba hiyo wakiwa wamejipanga katika miundo ya mapigano, walianza mashambulizi
kujibu mashambulio hayo.
Alisema
majibizano yaliendelea na watu hao waliokuwa wanashambulia kutoka ndani,
walivunja uzio na watu wanaokadiriwa kuwa zaidi ya watano walitoka huku wakiwa
wanashambulia.
Muroto
alisema askari waliendelea kupambana nao na kufanikiwa kuwajeruhi baadhi yao,
na wengine walifanikiwa kutoroka na silaha zao.
“Mashambulizi
kutoka ndani yalitulia na askari waliingia ndani ya uzio, kwa kuwa yalikuwa
mapambano ya nguvu walikuta majambazi watatu wanaokadiriwa kuwa na umri kati ya
miaka 25 na 30 wakiwa wamejeruhiwa kwa risasi na hali zao zilikuwa mbaya na
tuliwapeleka Hospitali ya Taifa Muhimbili lakini walibainika kuwa tayari
wameshakufa na miili yao imehifadhiwa hapo ikisubiri kutambuliwa,” alisema.
Alisema
baada ya kufanya upekuzi, polisi walikuta silaha moja aina ya short gun pump
action yenye MV.51516 R na namba ya usajili TZ car 99987 na risasi tano ndani
ya magazini yake.
Risasi
nyingine sita za short gun zilikutwa ndani ya mfuko wa plastiki pamoja na
risasi nane za pistol.
Aidha
alisema katika tukio hili, ilibainika kuwa kuna askari mmoja alijeruhiwa bega
lake la kushoto na lilikuwa jeraha kubwa la risasi, hivyo alipelekwa katika
Hospitali ya Muhimbili ambako amelazwa na anaendelea kupata matibabu akisubiri
kufanyiwa upasuaji.
Muroto
alisema ufuatiliaji wa majambazi, walitoroka eneo la mapambano uliendelea kwa
kushirikiana na wananchi wa kijiji cha Mtambani, ambapo majira ya saa tatu
asubuhi jambazi mmoja alipatikana akiwa mahututi na juhudi za kumfikisha
hospitali zilifanyika. Hata hivyo, alikufa akiwa njiani.
”Tunawashukuru
wananchi wote wema kwa ushirikiano mkubwa waliouonesha kwa Jeshi la Polisi, kwa
kuliunga mkono katika kufichua wahalifu na kupambana na wahalifu, nitoe
tahadhari kuwa mkoa huu ukifanya tukio ujue utashughulikiwa kabla hujakamilisha
na ukifanikiwa kukamilisha azma yako haitachukua muda utakamatwa,” alisisitiza.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ MAJAMBAZI MENGINE YAUAWA KATIKA MAPAMBANO MAKALI MKURANGA”
Post a Comment