Saturday, October 22, 2016
POLISI WATELEKEZA PIKIPIKI INAYOHUSISHWA NA USHIRIKINA
Do you like this story?
PIKIPIKI
yenye namba za usajili T 684 CJZ aina ya Fekon iliyotelekezwa kwa zaidi ya
mwaka mmoja katika kituo cha waendesha bodaboda cha Maganga Veterinary Temeke
jijini Dar es Salaam inazua hofu kwa wananchi na hata kwa askari polisi ambao
wameshindwa kuipeleka kituoni.
Imeelezwa
kwamba pikipiki hiyo iliegeshwa katika eneo hilo na mtu mmoja ambaye alifika
nayo akiwa akiiendesha mwishoni mwa mwaka jana.
Akizungumza
jana na mtandao wa www. habari za jamii.com mmoja wa waendesha bodaboda wa
kituo hicho ambaye hakupenda kujitambulisha jina lake alisema pikipiki hiyo
inawapa hofu wananchi wa eneo hilo na hata waendesha bodaboda.
“Hata
sisi wenyewe tuna hofu na pikipiki hii ndio maana tunaegesha mbalimbali na
pikipiki zetu na ndio maana sitaki kutaja jina langu” alisema mwendesha
bodaboda huyo.
Aliongeza
kuwa awali baada ya pikipiki hiyo kutelekezwa katika kituo hicho mtu yeyote
alipokuwa akiisogelea au kuigusa ilikuwa ikijiwasha yenyewe lakini baada ya
kupita mwezi mmoja iliacha kujiwasha jambo ambalo limeongeza hofu kwa wananchi.
Mkazi
mwingine wa eneo hilo aliyejitambulisha kwa jina moja la Ismail alisema hata
walipotoa taarifa kituo cha polisi cha Maganga walishindwa kuichukua pikipiki
hiyo kutokana na tabia ya kujiwasha.
Alisema
aaskari wa kituo hicho ambacho kipo mita 10 na eneo ambalo ipo pikipiki hiyo
walitoa taarifa kwa wenzao wa kituo cha Chang’ombe ambao nao wameshindwa
kuichukua na kwenda nayo kituoni kwa ajili ya kumtambua mmiliki wa pikipiki
hiyo kupitia namba zake za usajili.
Ismail
alisema inawezekana pikipiki hiyo ilifungwa kifaa maalumu cha utambuzi iwapo
kama imeibiwa na ndio maana ilipokuwa ikiguswa au kusogelewa inajiwasha yenyewe
licha ya baadhi ya watu wanahusisha kujiwasha kwake na imani za ushirikina.
Imeelezwa
kuwa pikipiki hiyo wakati inatelekezwa ilikuwa katika hali ya upya lakini hivi
sasa imeanza kupoteza upya wake kwa kukosa huduma ya matunzo.
Jitihada
za mtandao huu kumpata Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa huo wa Maganga ili
kuzungumzia suala hilo zimeshindika baada ya kuelekezwa alikuwa Manispaa ya
Temeke kwenye mkutano.
Na Dotto
Mwaibale
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ POLISI WATELEKEZA PIKIPIKI INAYOHUSISHWA NA USHIRIKINA”
Post a Comment