Tuesday, October 18, 2016

SERIKALI YAMRUDISHA KAZINI MKURUGENZI WALIYEMTUMBUA




Serikali imerejesha kazini Mkurugenzi Mkuu wa bodi ya pamba Tanzania Bwana Marco Mtunga baada ya kushindwa kupata uthibitisho wa tuhuma zilizokuwa zikimkabili za matumizi mabaya fedha kiasi cha  shilingi bilioni 2.4 zilizotakiwa kulipwa wakulima wa pamba walioathirika na mdororo wa uchumi wa mwaka 2008.

Akizungumza na waandidhi wa habari waziri wa kilimo,mifugo na uvuvi, Mhe Dkt Charless Tizeba pichani amesema Bwana Mtunga anakiwa kuripoti ofisini katika nafasi yake kuanzia sasa na kusisitizia serikali imejiridhisha tuhuma zilizokuwa zikimkabiri hazina ukweli wowote.

Aidha siku cha chache baada ya waziri kuu kuagiza kufanyika mabadiliko katika ya bodi ya Korosho, hatimaye serikali imemuondoa Kaimu Mkurugenzi wa bodi ya Korosho Bwana Mfaume Mohamed, na kaimu mkurugenzi wa masoko Bwana Juma Yusuf na kuwateua bwana Hassani Jarafu kuwa kaimu mkurugenzi mkuu wa bodi hiyo, pamoja na bwana Ray Mtangi kuwa kaimu mkurugenzi wa masoko, na kuwabadilisha wajumbe wote wa bodi.

Mhe Dkt Tizeba amesema serikali ya awamu ya tano inaendelea kuboresha utendaji katika maeneo mbalimbali ili kuongeza tija na ufanisi,pamoja na hatua kubwa ambazo zimefikiwa katika sekta ya korosho serikali bado inaamini kuwa inaweza kufanya vizuri zaidi, ambapo sasa bei ya korosho imepanda hadi kufikia shilingi elfu tatu na mia sita kwa kilo, huku pamba pamba ikiwa imefikiwa shilingi elfu tatu na mia tatu kiwango ambachi hakijawahi kufikiwa toka kilimo cha korosho na kuanza hapa nchni.

0 Responses to “ SERIKALI YAMRUDISHA KAZINI MKURUGENZI WALIYEMTUMBUA”

Post a Comment

More to Read