Tuesday, October 18, 2016

VIDEO: ALICHOKISEMA KOCHA JOSE MOURINHO BAADA YA KUTOKA SARE NA LIVERPOOL




Baada ya kumalizika kwa mchezo wa EPL kati ya Liverpool iliyokuwa mwenyeji wa Manchester United na timu hizo kutoka sare ya bila kufungana, kocha wa Man United, Jose Mourinho amezungumza kuhusu mchezo huo.

Mourinho amesema Liverpool alicheza vizuri lakini walifanikiwa kuwadhibiti na kuwafanya kushindwa kupata goli lakini pia wapinzani wao walikuwa na washambuliaji wa kawaida ambao walishindwa kuwaletea madhara licha ya kumiliki mpira kwa muda mrefu. 

“Liverpool ni timu nzuri sana, unaweza kusema ni jambo la mwisho la ajabu wanafanya katika kushambulia, lakini wana timu ambayo inacheza na kufikiri jinsi ya kuzuia,
“Tuliwazuia wao kucheza lakini bado walicheza vizuri katika eneo la kuzuia. Walimchezesha Emre Can na Jordan Henderson kwa sababu maalumu na walifanya hivyo kwa dakika 90. 

Walikuwa na wachezaji wa kawaida katika eneo la kushambulia lakini Can na Henderson walikuwa makini sana katika eneo lao,” alisema na kuongeza.

“Msimu uliopita United ilishinda hapa na Liverpool walikuwa na mashuti 14. Leo mangapi? mawili. Wameongoza takwimu kwa asilimia 65 na mashuti mawili. Jambo muhimu ni Liverpool sio sehemu yetu, ni matatizo yao, sio kosa letu”



0 Responses to “VIDEO: ALICHOKISEMA KOCHA JOSE MOURINHO BAADA YA KUTOKA SARE NA LIVERPOOL”

Post a Comment

More to Read