Tuesday, October 18, 2016
WATU 13 KIZIMBANI KWA MAUAJI YA WATAFITI DODOMA
Do you like this story?
Wanawake
wanne na wanaume tisa wamefikishwa mahakamani mjini Dodoma na kusomewa mashtaka
ya mauaji ya watafiti wa Chuo cha Utafiti wa Udongo na Maendeleo ya Ardhi
kilichopo Selian mkoani Arusha.
Mbele
ya Hakimu Mkazi, Joseph Fovo washtakiwa hawakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa
Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma haina mamlaka kisheria kusikiliza kesi hiyo
isipokuwa Mahakama Kuu.
Wanadaiwa
kuwaua Nicas Mag- azine, Theresia Nguma na Faraji Mafuru, Oktoba Mosi kwenye
Kijiji cha Iringa Mvumi wilayani Chamwino.
Wakili
wa Serikali, Beatrice Nsana aliwasomea mashtaka hayo jana akidai walitenda kosa
hilo la jinai kinyume na kifungu cha 196 na 197 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu
na marekebisho yake ya mwaka 2002.
Washtakiwa
hao ni Cecilia Mwalu, Dorca Mbehu, Edna Nuno, Grace Masaulwa, Juma Madeha,
Albert Chimanga, Sosteness Mseche, Julius Chimanga, David Chimanga, Lazaro Kwanga,
Yoramu Samamba, Edward Lungwa na Simon Samamba, wote wakazi wa Kijiji cha
Iringa Mvumi.
Kesi hiyo namba 36/2016 iliahirishwa hadi Oktoba 31. Nsana alidai upelelezi haujakamilika.
Kesi hiyo namba 36/2016 iliahirishwa hadi Oktoba 31. Nsana alidai upelelezi haujakamilika.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ WATU 13 KIZIMBANI KWA MAUAJI YA WATAFITI DODOMA”
Post a Comment