Thursday, October 6, 2016

TAARIFA YA AWALI YA TUKIO LA KUPIGWA MWANAFUNZI WA MBEYA DAY NDUGU SEBASTIAN CHINGULU






Tukio lilianza tarehe 26/9/2016 mwalimu Frank Msigwa mwanafunzi kwa vitendo toka Chuo Kikuu cha  Dar Es  salaam (DUCE) kutoa assignment ya soma la kingereza kwa wanafunzi wa kidato cha Tatu

Baada ya kusahihisha aligundua kuwa kuna baadhi ya wanafunzi hawakufanya NA tarehe 28/9/2016 alikwenda darasani NA kutoa adhabu NA alianza kwa kuwapa adhabu ya push up , kupiga magoti NA baadae viboko 2 katika utekelezaji mwanafunzi  Sebastian Chingulu alikataa kufanya  kutokana NA kuumwa na goti

Baada ya kukataa adhabu Mwl Frank Msigwa na wenzake 3, John Deo (DUCE), Sanke Gwamaka ( DUCE) na Evance Sanga( MWL Nyerere) walimpeleka ofisini na kuanza kumshambulia kwa kipigo na baada ya tukio hilo walitoeka na wakati wanamshambulia mwalimu mwingine aliwasihi wasimpige na alirekodi tukio hilo
Serikali ya mkoa inaendelea kuwashikilia walimu na mwalimu mkuu kwa mahojiano, kupata maelezo ya wanafunzi waliopata adhabu na mwanafunzi aliyepigwa

Nawahakikishia serikali itawasaka popote walipo walimu hawa waliofanya tukio hili  na kufikishwa katika vyombo vya dola na sheria
Aidha mwanafunzi aliyepigwa anaendelea kupimwa na matibatbu
Hii Ni taarifa ya awali nitaendelea kutoa taarifa kwa kila hatua
Amos G Makalla
RC  Mbeya
 






0 Responses to “TAARIFA YA AWALI YA TUKIO LA KUPIGWA MWANAFUNZI WA MBEYA DAY NDUGU SEBASTIAN CHINGULU ”

Post a Comment

More to Read