Sunday, October 23, 2016

TUZO YA KICHUYA YANOGESHA USHINDI WA SIMBA DHIDI YA TOTO AFRICAN.





Klabu ya Simba leo imeendeleza moto wake wa ushindi katika mechi za ligi kuu huku leo ikiichapa klabu ya Toto African kwa mabao 3 - 0.
Magoli ya Simba yalifungwa na kiungo wake Mzamiru katika kipindi cha kwanza dakika ya 42 na dakika ya 74 kipindi cha pili, huku mshambuliaji wake wa kimataifa Laudit Mavugo akifunga goli moja kwenye kipindi cha pili dakika ya 57.

Huku Simba wakirudi nyumbani na ushindi wa pointi tatu, Shiza Kichuya rasmi leo amekabidhiwa tuzo ya mchezaji bora kwa mwezi Septemba, 2016 ikiambatana na  fedha taslim laki tano. Tuzo hiyo imekabidhiwa rasmi kwa Kichuya na Makamu wa Rais wa klabu ya Simba Geophrey Nyange Kaburu.




Wiki iliyopita Kichuya alitangazwa tena na Bodi ya ligi kama mchezaji bora wa ligi kwa mwezi Septemba.

Fahari News inampongeza Kichuya kwa kuweza kushinda tuzo za ligi pomoja na ya ndani ya klabu yake ya Simba.

0 Responses to “TUZO YA KICHUYA YANOGESHA USHINDI WA SIMBA DHIDI YA TOTO AFRICAN.”

Post a Comment

More to Read