Wednesday, October 19, 2016
UBALOZI WA NORWAY WASAINI MKATABA WA BIL 10.6 NA UN KWAAJILI YA KUWASAIDIA WAKIMBIZI, KIGOMA
Do you like this story?
Kwa
kutambua hali ya kimaisha ambayo inawakabili wakimbizi waliopo mkoani Kigoma,
ubalozi wa Norway nchini umesaini mkataba wenye thamani ya dola milioni 4.8
(Tsh. Bilioni 10.6) na Umoja wa Mataifa (UN) kupitia Mpango wa Misaada ya
Maendeleo (UNDAP 2) kwa ajili ya kuwasaidia wakimbizi waliopo nchini.
Akizungumza
katika hafla ya utiliaji saini mkataba huo, Balozi wa Norway ncini, Hanne-Marie
Kaarstad alisema pesa ambazo wamezitoa zinalenga zaidi kuwasaidia wakimbizi
waliopo Kigoma ili waweze kuwa na shughuli za kuwasaidia na hasa kwa wanawake
na watoto.
“Kwetu ni
jambo muhimu kushirikiana na UN kwa ajili ya kuwalinda watu ambao wanaingia
nchini kutoka nchi jirani, tulichangia katika mpango wa kwanza wa misaada ya
maendeleo na sasa tumejiunga katika mpango mwingine wa maendeleo wa 2016-2021,
“Tunafahamu
Kigoma mwaka jana mwezi Mei ilipokea wakimbizi wengi kutoka Burundi na sasa
tunaona ni vyema tukishirikiana na mashirika ya UN ili kuwasaidia na zaidi kwa
wanawake na watoto na wote tunatambua kuwa wanawake ndiyo chanzo kikuu cha
uchumi na hili sio Kigoma tu, maeneo yote ipo hivyo,” alisema Kaarstad.
Nae
Mratibu Mkuu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa (UN), Alvaro Rodriguez alisema ni
jambo zuri kuona Norway inaendeleza ushirikiano na Tanzania na wao wamejipanga
kuhakikisha wakimbizi wanaokusudiwa kunufaika na pesa hizo zinawafikia na
kufanya kazi ambayo zimepangiwa kufanyika.
“Tunajivunia
ushirikiano imara wa UN na Norway kwa kuwa tayari kusaidia watoto na wanawake ,
Norway imekuwa ikisaidia Tanzania na leo ni heshima kuona wakisaidia kwa mara
nyingine,
“Sehemu
ambazo zinakuwa na wakimbizi zina changamoto zake na hata kwa nchi kunapokuwa
na wakimbizi kunashughuli za kijamii zinakuwa zinasimama, sisi kama UN
tutashirikiana na serikali kufanya ambacho mnakilenga na kufikia malengo
yaliyowekwa hadi 2021,” alisema Rodriguez.
Aidha
alisema msaada ambao umetolewa na ubalozi wa Norway utatekelezwa sambamba na
malengo ya dunia ambayo ni pamoja na kumaliza umaskini, usawa wa kijinsia na
uhifadhi wa mazingira.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ UBALOZI WA NORWAY WASAINI MKATABA WA BIL 10.6 NA UN KWAAJILI YA KUWASAIDIA WAKIMBIZI, KIGOMA”
Post a Comment