Monday, November 7, 2016
HII HAPA TAARIFA YA JESHI LA POLISI AJALI YA NOAH ILIYOUA WATU 18 SHINYANGA
Do you like this story?
AFANDE RC TAARIFA YA (M) SHINYANGA KWA SAA 12 ZILIZOPITA
(1) AJALI YA GARI KUGONGANA NA KUSABABISHA VIFO SHY/TR/AR/185/16.
06/11/2017 MAJIRA KATI YA 1900 - 1930HRS KATIKA BARABARA YA NZEGA - TINDE, KATIKA KIJIJI CHA NSALALA KATA YA TINDE WILAYA NA MKOA WA SHINYANGA GARI NA T 232 BQR TOYOTA NOAH MALI YA MWINYI KHAMIS WA TINDE IKIENDESHWA NA SEIF S/O MOHAMED, 32YRS, SUKUMA NA MKAZI WA TINDE, IKITOKEA NZEGA KWENDA TINDE ILIGONGANA USO KWA USO NA SEMI TELLER T198 CBQ/T283 CBG ILIYOKUWA IKITOKEA TINDE UELEKEO WA NZEGA MALI YA ALOYCE S/O KAVISHE, MCHAGA, 46YRS MKAZI WA DSM NA AMBAYE PIA ALIKUWA DEREVA WA GARI HILO NA KUSABABISHA VIFO VYA WATU 18.
KATI YAO WANAUME 7 , WANAWAKE 9 NA WATOTO 02 WAKIKE WENYE UMRI WA KATI YA MIAKA 3- 5, MIILI YA MAREHEMU IMEHIFADHIWA HOSPITAL YA RUFAA YA MKOA WA SHINYANGA.
TUKIO HILI LIMEKAGULIWA NA ACP J. MULIRO KAMANDA MKOA WA SHINYANGA, SSP MWAKISAMBWE - RCO SHINYANGA NA SP ANTONY MASANZU - RTO SHY AKISAIDIWA NA DTO SHY ASP ANTONY GWANDU.
MADEREVA WOTE MBARONI KWA MAHOJIANO YA TUKIO HILO NA HATUA ZA ZAIDI ZA KISHERIA.
CHANZO CHA AJALI HII KWA TAARIFA ZA AWALI NI UZEMBE WA DEREVA WA NOAH KUAMUA KUYAPITA MAGARI YALIYOKO MBELE YAKE BILA KUCHUKUA TAHADHARI NA HATIMAE KUGONGANA USO KWA USO NA LORI - SEMITELLAR. MAREHEMU WATATU WAMETAMBULIWA.
(2) MAKOSA YA USALAMA BARABARANI YAMEKAMTWA 167, YOTE YA MELIPWA, MADUHURI YALIYOKUSANYWA TSH 4,990,000/=,
3.AFYA ZA ASKARI NA WATUMISHI RAIA KWA UJUMLA NI NZURI.
Watu
18 wamefariki dunia na watatu kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha gari aina ya
Noah iliyokuwa inatoka Nzega mkoani Tabora kuelekea Tinde mkoani Shinyanga na
lori aina ya Scania lililokuwa linatoka Kahama kuelekea Dar es salaam.
Ajali hiyo imetokea leo Jumapili,November 06,2016 majira ya mbili kasorobo usiku katika eneo la Nsalala kata ya Tinde mkoani Shinyanga (Barabara ya Nzega- Shinyanga).
Ajali hiyo imetokea leo Jumapili,November 06,2016 majira ya mbili kasorobo usiku katika eneo la Nsalala kata ya Tinde mkoani Shinyanga (Barabara ya Nzega- Shinyanga).
"Noah ilikuwa inataka kulipita lori jingine ndipo ikagongana uso kwa uso na lori lililokuwa linatoka Kahama... watu waliopoteza maisha papo hapo ni 15,watatu wamefariki wakati wakipatiwa matibabu,ajali inatisha,dereva wa Noah kajisalimisha kituo cha polisi Tinde",kimesema chanzo cha habari cha Malunde1 blog.
Majeruhi wamekimbizwa hospitali ya mkoa wa Shinyanga.
![]() |
Miili ya watu waliofariki dunia katika ajali ya Noah kugongana na lori |
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “HII HAPA TAARIFA YA JESHI LA POLISI AJALI YA NOAH ILIYOUA WATU 18 SHINYANGA ”
Post a Comment