Monday, November 7, 2016
TAKUKURU YAJITOSA KUCHUNGUZA TUHUMA ZA WABUNGE WA CCM KUHONGWA MILIONI 10
Do you like this story?
Taasisi
ya Kuzuia na Kupambanana Rushwa (Takukuru) imeanza kuchunguza tuhuma
zilizoibuliwa Bungeni kuwa Wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) walipewa rushwa
ya shilingi milioni 10.
Tuhuma
hizo zilitolewa wiki iliyopita Bungeni na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani,
Freeman Mbowe alipomuuliza swali Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
Hata hivyo, swali lake halikupata jibu ndani ya jengo hilo baada ya kuwekewa zuio na Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson alieleza kuwa halikuwa swali la kisera.
Hata hivyo, swali lake halikupata jibu ndani ya jengo hilo baada ya kuwekewa zuio na Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson alieleza kuwa halikuwa swali la kisera.
Mbowe
alitaka kufahamu kutoka kwa Waziri Mkuu kama tuhuma hizo ni za kweli au la,
akidai fedha hizo zilitolewa kwa lengo la kuwashawishi kupitisha muswada wa
sheria ya huduma za habari na mpango wa maendeleo ya taifa.
Mkurugenzi
Mkuu wa Takukuru, Valentino Mlowola amesema kuwa taasisi hiyo imeanza uchunguzi
kama alivyosema Rais John Magufuli alipokuwa akijibu swali katika mkutano wake
na vyombo vya habari mwishoni mwa juma lililopita, Ikulu jijini Dar es Salaa.
“Ndiyo,
tumeanza kuchunguza, Takukuru ni chombo chake na tumeanza kazi hiyo,” Mlowola anakaririwa .
Mkuu
huyo wa Takukuru alifungua mlango kwa yeyote mwenye ushahidi kuhusu tuhuma hizo
aziwasilishe ili kukisaidia chombo hicho.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “TAKUKURU YAJITOSA KUCHUNGUZA TUHUMA ZA WABUNGE WA CCM KUHONGWA MILIONI 10”
Post a Comment