Saturday, November 5, 2016
MAJIBU YA JPM KWA WANAHABARI KUHUSU MUSWAADA WA SHERIA YA HUDUMA ZA HABARI 2016
Do you like this story?
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Magufuli amesema kuwa
huu ni wakati mwafaka kwa muswada wa sheria ya huduma za vyombo vya habari
kukubaliwa na kuwa sheria kwa vile tasnia ya habari inakumbwa na changamoto
nyingi zitakazotatuliwa na sheria hiyo.
Akizungumza
na wahariri pamoja na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari jana, Ikulu
jijini Dar es Salaam Rais Magufuli alisema kuwa muswada huo ni wa muda mrefu na
sasa ni wakati mwafaka kwa vile tansia ya habari inakumbwa na changamoto nyingi
zinazoweza kutatuliwa na muswada huo.
“Hii
sheria ya huduma za vyombo vya habari imechelewa kwa vile mchakato wake ulianza
tangu mwaka 2011 hadi sasa mwaka 2016 wadau walikuwa na muda wa kutosha wa
kujiandaa na kutoa maoni yao ambayo yangeweza kuboresha muswada huo” alisema Rais Magufuli
Ameongeza
kuwa, Sheria hii italeta mabadiliko katika tasnia ya habari kwa vile kutakuwepo
na Bodi ambayo itashughulikia masuala ya taaluma ya habari, pamoja na mambo
mengine yaliyoanishwa katika muswada huo ambayo ni maslahi ya waandishi wa
habari nchini.
Muswada
huu unatazamiwa kuwajengea uwezo waandishi wa habari ili waweze kufanyakazi
kitaalamu kwa kuandika na kutangaza habari zenye ukweli zitakazochangia katika
harakati za kuleta maendeleo kwa nia ya kuwasaidia watanzania na serikali kwa
ujumla katika kufikia malengo yake.
Muswada
wa Sheria ya huduma za habari umesomwa jana Novemba 4, 2016 katika kikao cha
tano cha Bunge na mkutano wa 11, ambapo utajadiliwa na kufuata taratibu zingine
kabla ya kuwa sheria.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
.gif)


0 Responses to “ MAJIBU YA JPM KWA WANAHABARI KUHUSU MUSWAADA WA SHERIA YA HUDUMA ZA HABARI 2016”
Post a Comment