Saturday, November 5, 2016
VIZA ZA ISRAEL ZAANZA KUTOLEWA HAPA NCHINI,FAIDA ZAKE ZABAINISHWA
Do you like this story?
Serikali
ya Israel imeanza kutoa huduma za viza moja kwa moja kutokea jijini Dar es
Salaam ambapo kwa mujibu wa Waziri wa Maliasili na Utalii Profesa Jumanne
Maghembe, hatua hiyo itachochea ukuaji wa biashara pamoja na ushirikiano wa
kidiplomasia.
Awali,
viza zilikuwa zikitolewa jijini Nairobi nchini Kenya lakini hivi sasa huduma
hiyo itakuwa ikipatikana jijini Dar es Salaam ambapo Waziri Maghembe ametaja
baadhi ya faida chache za utolewaji wa huduma hizo hapa nchini kuwa ni kupungua
kwa urasimu na gharama za kutafuta viza, kukua kwa ushirikiano katika nyanja
zote za uchumi, elimu ulinzi pamoja na usalama.
Balozi
wa Israel nchini Kenya Bw. Yahel Vilan amesema hatua hiyo itakuza uhusiano wa
kidiplomasia hususani kwenye eneo la uchumi, kutokana na uzoefu mkubwa iliyonao
taifa hilo ambalo hivi sasa limepiga hatua kubwa kwenye uchumi na teknolojia.
Kwa
upande wake, Bi. Pooja Lalji amesema wamejipanga kuhakikisha wafanyabiashara
wanaokwenda Israel wanapata viza zao mapema na hivyo kuchochea biashara baina
ya Tanzania na taifa hilo la Mashariki ya Kati
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
.gif)

0 Responses to “ VIZA ZA ISRAEL ZAANZA KUTOLEWA HAPA NCHINI,FAIDA ZAKE ZABAINISHWA”
Post a Comment