Wednesday, November 2, 2016
SERIKALI YAAHIDI KULIPA NGUVU JESHI LA POLISI KUKABILIANA NA WALIFU
Do you like this story?
Waziri wa
mambo ya ndani, Mwigulu Nchemba, amesema serikali inatambua umuhimu wa askari
polisi na ndio maana ina mkakati wa kuliwezesha jeshi hilo vitendea kazi bora.
Waziri Nchemba ameyasema hayo Jumatano hii alipokuwa akitoa
ufafanuzi wa matukio ya kuvamiwa kwa askari kujeruhiwa au hata kuuawa.
“Serikali inatambua umuhimu wa askari polisi, wanapokuwa katika
kutimiza majukumu yao ya kila siku. Napenda kulihakikishia bunge lako tukufu
kwamba serikali itaendelea kuliwezesha jeshi la polisi hapa nchini kwa vitendea
kazi bora na kuwajengea uwezo askari wetu kwa mafunzo ili waweze kukabiliana na
matukio ya uhalifu yanayohusisha uvamizi wa askari polisi,” alisema Nchemba.
“Kwa sehemu ya pili jeshi la polisi limefanikiwa kukamata silaha
19 kati ya 23 zilizoporwa kutoka kwa askari waliovamiwa wakiwa katika majukumu
yao katika kipindi cha Julai 2015 hadi Septemba 2016,” aliongeza.
BY: EMMY MWAIPOPO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
.gif)


0 Responses to “ SERIKALI YAAHIDI KULIPA NGUVU JESHI LA POLISI KUKABILIANA NA WALIFU”
Post a Comment