Monday, November 7, 2016
WALIOKULA FEDHA ZA MIKOPO ELIMU YA JUU KITANZINI.....SHERIA YAREKEBISHWA KUWABANA ZAIDI.
Do you like this story?
Muswada
wa Sheria ya Mabadiliko ya Sheria Mbalimbali Namba 3 wa Mwaka 2016 unatarajiwa
kuwasilishwa bungeni leo, ukigusa sheria tisa ikiwemo ya Mikopo kwa Wanafunzi
wa Elimu ya Juu ambapo sasa mnufaika wa mkopo aliyejiajiri atalipa kiasi
kisichopungua Sh 120,000 au asilimia 15 ya kipato chake, huku taasisi za umma,
bodi, wakala na tume zimebanwa zisirekebishe au kuwianisha mishahara, posho na
marupurupu kwa watumishi.
Kwa
mujibu wa muswada huo, kwenye Sheria ya Mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu,
waajiri wanaoshindwa kuwasilisha marejesho ya mwezi baada ya makato
wataadhibiwa, ambapo mwajiri atawajibika kuitaarifu Bodi ya Mikopo kuhusu ajira
ya mtu yeyote ambaye ana shahada au stashahada na kukata makato ya mwezi kutoka
kwenye mshahara wa mnufaika wa mkopo.
Kifungu
hicho kinapendekeza kufanya marejesho ya mkopo kuwa ya kisheria na kupewa
nafasi ya awali katika orodha ya makato na kinapendekeza kupunguzwa idadi ya
wajumbe wa Bodi ya Mikopo na kufikia saba kwa lengo la kupunguza gharama za
uendeshaji.
Kwenye
marekebisho ya Sheria ya Utumishi wa Umma, Kifungu cha 8 kinapendekeza
kufanyiwa marekebisho ili kumpa mamlaka Katibu Mkuu (Utumishi) kurekebisha na
kuwianisha mishahara, posho na marupurupu mengine kwa watumishi wa umma.
Inapendekezwa
kumuondolea Katibu mamlaka ya kuteua watumishi wa umma wanaounda baraza la
majadiliano ya pamoja ya watumishi wa umma na sasa waziri atateua katibu kutoka
wizara yenye dhamana na kada husika ya watumishi.
Pia
inapendekezwa kufuta kifungu cha 11 ili kuondoa masharti yanayokataza Baraza la
majadiliano ya pamoja ya watumishi na baraza la pamoja la watumishi wa umma
kutoa mapendekezo kuhusu ujira.
Kwa
upande wa marekebisho ya Sheria ya Leseni na Usafirishaji, Mamlaka ya Udhibiti
Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) kutaongezwa kifungu ili kuweka
masharti yanayoruhusu ulipwaji wa faini pale mkosaji anapokiri kosa, badala ya
kila kosa kufuata taratibu za kimahakama.
Muswada
huo una marekebisho kwenye Sheria ya Mazingira ambako kutawekwa mwongozo wa
namna ya kupima urefu wa mita 60 kwenye kingo za bahari, ziwa, mto au bwawa la
maji kinachozuiliwa kufanyia shughuli zozote za binadamu. Upimaji utapimwa
kuanzia kwenye kingo za maeneo hayo.
Sheria
nyingine zitakazofanyiwa marekebisho kwenye Mkutano wa Tano wa Bunge la 11 ni
ya Usafiri wa Anga, Sheria ya Msajili wa Hazina na Sheria ya Vipimo.
Spika
Job Ndugai wakati akizungumza na waandishi wa habari kabla ya kuanza kwa
Mkutano wa Tano wa Bunge wiki iliyopita, alieleza kuwa kwa wiki hii Bunge
litapokea taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali(CAG) ya mwaka
2014/2015 kisha kujadili na kuishauri serikali kuhusu Mkataba wa Ushirikiano wa
Kiuchumi kati ya Jumuiya ya Ulaya (EU) na Afrika Mashariki (EPA-EU) na kisha taarifa
ya kamati ndogo kuhusu uchambuzi wa sheria ndogo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “WALIOKULA FEDHA ZA MIKOPO ELIMU YA JUU KITANZINI.....SHERIA YAREKEBISHWA KUWABANA ZAIDI.”
Post a Comment