Wednesday, February 22, 2017
CAMERA ZAMPONZA WAYNE SHAW
Do you like this story?
Meneja wa klabu ya Sutton United Paul Doswell amethibitisha taarifa za kujiuzulu kwa kipa wake Wayne Shaw ambaye ameanza kufanyiwa uchunguzi na chama cha soka nchini England FA.
Shaw jana alipamba kurasa za mbele za magazeti ya nchini England, baada ya kuonekana akipata msosi wakati mchezo wa 16 bora wa kombe la FA kati ya Sutton united dhidi ya Arsenal ambao walichomoza na ushindi wa mabao mawili kwa sifuri.
Doswell alithibitisha taarifa za kujiuzulu kwa mlinda mlango huyo alipozungumza na kituo cha televisheni cha Sky News, ambapo amesema ilimsikitisha kuona kitendo cha mchezaji wake akila bagger akiwa kwenye benchi la wachezaji wa akiba.
“Nafikiri kitendo hicho kimemfanya kuwa nyota kwa kipindi kifupi, japo hakikunipendeza, kwa sababu sio desturi kwa wanchezaji kula wanapokua kwenye benchi.,” Alisema.
“Sio kawaida yake kufanya kitendo kama kile, lakini kwa bahati mbaya kimekuzwa na vyombo vya habari na imemlazimu kuamua kujiweka pembeni na mchezo wa soka, kupisha uchunguzi wa FA ambao ulianza mara moja.” Aliongeza Doswell.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “CAMERA ZAMPONZA WAYNE SHAW”
Post a Comment