Wednesday, February 22, 2017
MAN UTD YAACHA ATHARI EWOOD PARK
Do you like this story?
Kichapo cha mabao mawili kwa moja kilichotolewa na mashetani wekundu dhidi ya Blackburn Rovers mwishoni mwa juma lililopita, kimeacha athari kwa meneja Owen Coyle.
Man Utd walishinda mchezo huo wa kombe la FA, kupitia kwa washambuliaji Marcus Rashford na Zlatan.
Uongozi wa Blackburn Rovers umeonyesha kuchukizwa na matokeo hayo na kuyajumuisha kwenye mlolongo wa udhaifu wa meneja Owen Coyle, ambaye alikabidhiwa jukumu la kuwa mkuu wa benchi la ufundi tangu mwaka 2016.
Jana uongozi huo ulitangaza kuvunja mkataba na meneja huyo kutoka nchini England, baada ya kujiridhisha hatokua na uwezo wa kuendelea kupata matokeo mazuri katika kipindi cha msimu kilichosalia.
Matokeo ya michezo ya ligi daraja la kwanza ambapo Blackburn wanashiriki kwa sasa, nayo yamechangia kwa kiasi kikubwa maamuzi hayo kuchuliwa.
Rovers ambao walikua mabingwa wa England msimu wa 1994/95 hawajawahi kufanya vizuri kwa zaidi ya miaka 20, na msimu huu wapo kwenye janga la kushuka daraja kwa kuendelea kusota kwenye nafasi ya 23 miongoni mwa timu 24 zinazoshiriki ligi daraja la kwanza.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MAN UTD YAACHA ATHARI EWOOD PARK”
Post a Comment