Thursday, February 23, 2017

DAKTARI ATOA USHAHIDI JINSI SCORPION ALIVYOMTOBOA UTUMBO MRISHO



SHAHIDI katika kesi inayomkabili Salum Njwete maarufu ‘Scopion’, Daktari wa Kitengo cha Upasuaji cha Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dk. Amin Abdulrahman ameiambia mahakama kuwa Saidi Mrisho alitobolewa utumbo mwembamba.
Akitoa ushahidi mbele ya hakimu Flora Haule Dk. Abdulrahmani alisema Septemba 7, mwaka jana saa 12 alfajiri akiwa chumba cha upasuaji alipigiwa simu na kitengo cha dharura cha hospitalini hapo kumtaka kwenda kumhudumia mgonjwa wa dharura.
“Baada ya kumfanyia uchunguzi niligundua anahitaji kufanyiwa upasuaji kutokana na jeraha kubwa lililokuwa kushoto mwa tumbo lake lililokuwa na urefu wa sentimita 30 kutoka katika ngozi ya ndani ya tumbo lililotoboa utumbo mwembamba na mengine madogo ambayo yalishonwa na kitengo cha dharura,” alisema Dk. Abdulrahman.
Alisema alifungua tumbo na kuliziba tundu hilo kasha kufunga tumbo na kumpeleka wodi namba 13 na kumpa rufaa kwa wataalamu wa macho kuendelea na uchunguzi wa majeraha ya machoni. Kesi hiyo itatajwa tena Machi 8, mwaka huu.

0 Responses to “DAKTARI ATOA USHAHIDI JINSI SCORPION ALIVYOMTOBOA UTUMBO MRISHO”

Post a Comment

More to Read