Thursday, February 23, 2017

MAJANGA TENA,MAITI YAZIKWA KIMAKOSA KATAVI,MAHAKAMA YAAGIZA IFUKULIWE


Wananchi wa mkoani Katavi wamelazimika kuandamana ili kupewa mwili wa ndugu yao aliyefariki dunia akipatiwa matibabu katika hospitali ya manispaa ya Mpanda mkoani Humo

Mwili huo wa Marehemu Mathias Madega ulizikwa kimakosa na Manispaa baada ya kutolewa na msimamizi wa hospitali hiyo kimakosa wakidhani ni mwili wa mtua ambaye hakutambuliwa

Wakizungumza kwa masikitiko ndugu wa marehemu waliojitambulisha kwa majina ya Beatus Konji na Suzana Joseph wamesema walikuwa wakizungushwa na kutopewa majibu ya kuridhisha na madaktari hali iliyowafanya washindwe kuelewa sababu za kupewa maiti iliyokaa katika chumba cha kuhifadhia maiti kwa muda mrefu badala ya ule wa ndugu yao unaokaribia siku 14

Mama Mzazi wa marehemu Rehema Edward ameeleza namna alivyodai mwili wa mwanae na kupewa kibali na mahakama cha kufukua maiti hiyo na kwenda kuizika tena


Kufuatia mkanganyiko huo Mkurugenzi Mtendaji wa manispaa ya Mpanda Michael Francis ameahidi kuchukua hatua kwa aliyehusika kufanya makosa hayo na kwa sasa anasubiri ripoti ya uongozi wa hospitali CHMT

0 Responses to “MAJANGA TENA,MAITI YAZIKWA KIMAKOSA KATAVI,MAHAKAMA YAAGIZA IFUKULIWE ”

Post a Comment

More to Read