Thursday, February 23, 2017
WANIGERIA WATOA KAFARA YA KUMPOTEZA RAIS BUHARI
Do you like this story?
Ukistaajabu ya Musa utayaona ya firauni
ndivyo unavyoweza kusema kwa kinachomtokea kwa sasa Rais wa Nigeria,
Muhammadu Buhari ambaye yupo nchini Nigeria akipatiwa matibabu baada ya
kikundi cha Shiite Islamic kutoa kafara ili tu apoteze maisha akiwa
hukohuko kabla ya kurejea nchini kwake.
Kikundi hicho kimetoa kafara ya ng’ombe
na kusoma dua ili Rais Buhari hali yake ya kiafya izidi kuwa mbaya kwa
jinsi siku zinavyozidi kwenda akiwa kwenye matibabu na baadae afe kabisa
kabla hajarejea Nigeria.
Maombi hayo yalifanyika katika mji wa
Borno na sababu ya kikundi cha Shiite Islamic kufanya hivyo inatajwa
kuwa ni kutopendezwa na utendaji kazi wa Buhari jinsi anavyoongoza
serikali yake na hivyo kwao ni vyema kama akifa ili asiwepo kabisa.
Hali ya kiafya ya Buhari bado
haijawekwa wazi kwa sasa inaendelea lakini wiki iliyopita, Msemaji wake
alisema anataraji kurejea Nigeria siku za karibuni na hakutakuwa na
mapokezi yoyote ambayo yatafanyika kwa Rais huyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “WANIGERIA WATOA KAFARA YA KUMPOTEZA RAIS BUHARI”
Post a Comment