Wednesday, March 29, 2017
ATUPWA JELA MIAKA 5 KWA KUMFUNGA MBWA WAKE KAMBA MDOMONI
Do you like this story?
Mwanamume
mmoja alietambulika kwa jina la William Dodson (43) raia wa Marekani
ambaye alimfunga mbwa wake mdomoni kwa kamba, amehukumiwa kifungo cha
miaka mitano jela.
Anasema
alimfunga mbwa huyo mdomoni kwa sababu alibweka sana ndipo alipoamua
kufunga mbwa huyo mpaka kumsababishia kupoteza sehemu ya ulimi wake. ,
jambo ambalo lilisababisha mbwa huyo kufanyiwa upasuaji mara kadha.
Kamba
aliyotumia kumfunga mbwa hiyo ilizuia damu kufika hadi kwenye ulimi
wake, na iliwachukua madaktari wa mifugo karibu saa 36 kuiondoa.
Mbwa
huyo aliyejulikana kwa jina la Caitlyn, alifanikiwa kutoroka mwezi Mei
mwaka 2015, na alikuwa mgonjwa sana wakati alipatikana akirandaranda
barabarani
Caitlyn, alikuwa na umri wa miezi 15 wakati alipatikana na sasa amehitimu miaka mitano akiwa anaishi na familia tofauti.
Wakati
huo chama cha wanyama cha Charleston, kibadilisha picha ya akaunti yake
na kuweka picha ya mbwa hiyo, kama njia ya kuonyesha uzalendo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)