Wednesday, March 29, 2017
WAKAZI WA NJOMBE WAHIMIZWA KUCHANGIA DAMU
Do you like this story?
Katibu
Tawala wilaya ya Njombe, Joseph Chota amewahimiza wakazi wa mkoa wa
Njombe kujitolea kuchangia damu salama ili kusaidia watu wenye mahitaji.
Akizungumza
kwa niaba ya mkuu wa mkoa katika maadhimisho ya wiki ya matendo ya
huruma ya kanisa la Waadventista Wasabato mkoni Njombe, Chota amesema
damu itakayochangwa pia itasaidia kukabiliana na tatizo la uhaba wa damu
salama katika bohari za dawa hospitalini.
Waumini
wa kanisa la Waadventista Wasabato Duniani kote huadhimisha siku ya
matendo ya huruma kwa kuisaidia jamii kutatua changamoto mbalimbali
ikiwa ni sehemu ya ibada na kumtukuza Mungu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)