Wednesday, March 29, 2017

MALECELA AFUNGUKA MAKUBWA


Askari na Maafisa wa jeshi la Polisi nchini, wameaswa kutotumia madaraka yao vibaya ikiwa ni pamoja na kuwatumika Watanzania wote kwa upendo moyo mmoja.

Hayo yalisemwa jana na Waziri Mkuu Mstaafu, Mzee John Malecela wakati akizungumza kwenye ufunguzi wa kikao cha kazi cha Siku tatu cha mwaka 2017 kwa maafisa waandamizi wa Polisi na Makamanda wa Mikoa/Vikosi kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa LAPF Mjini Dodoma.
Mzee Malecela alisema; 

“Tulipopata uhuru na Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, alisema, Watanzania tumepata uhuru, hatuna uwezo wa kunyesha hela kama mvua kutoka mbinguni, umaskini utaendelea kuwepo.

“Lakini jambo moja la uhakika tunaloweza kumfanyia Mtanzania huyu, ni kuhakikisha tunapata heshima yake.

“Heshima ni kitu ambacho serikali inaweza kumpa kila Mtanzania…

0 Responses to “MALECELA AFUNGUKA MAKUBWA”

Post a Comment

More to Read