Wednesday, March 29, 2017
WAPANDISHWA MAHAKAMANI KISUTU KWA KUINGIZA MAKONTENA YA MITUMBA YENYE MAGARI
Do you like this story?
Wafanyabiashara
watatu wanaotuhumiwa kuingiza nchni makontena ya mitumba yaliyokuwa na
magari wamefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu na kushindwa
kusomewa hati ya makosa baada ya upande wa mashtaka kufanyia mabadiliko
ya hati ya mashtaka.
Wafanyabishara
hao walifika mahakamani hapo majira ya asubuhi na kukaa mahakamani hapo
kwa zaidi ya masaa sita wakiwa chini ya ulinzi na hatimaye kurudishwa
polisi ili kupisha muda wa kufanyia mabadiliko hati ya mashtaka.
Akizungumza
na vyombo vya habari mmoja wa wakili wa watuhumiwa hao amedai kuwa
wateja wake wamelazimika kurudishwa mahabusu kutokana na mabadiliko hayo
ya hati ya mashtaka.
Amesema
wateja wake wameshikiliwa na polisi kwa muda mrefu na uenda
wakafikishwa mahakamani hapo kesho kama upande wa mashtaka utafanikiwa
kufanya mabadiliko hayo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)