Monday, March 27, 2017
HABARI KUTOKA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI NEC
Do you like this story?
Mwenyekiti
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Mhe. Jaji (R) Semistocles Kaijage
amewataka watumishi wa tume hiyo wazingatie maadili na kanuni za utawala
bora ili kutekeleza kwa ufanisi jukumu la Tume katika kukuza na
kuimarisha demkorasi na utawala bora nchini.
Jaji
Kaijage ameyasema hayo alipoalikwa kuwa mgeni rasmi kufungua kikao cha
Baraza la Wafanyakazi wa Tume kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano
wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima jijini Dar es Salaam.
“Jukumu
kubwa la Tume ni kukuza na kuimarisha demkorasi na utawala bora nchini,
kwa maana hiyo ni muhimu kwamba watumishi wa Tume wazingatie maadili na
kanuni za utawala bora ili kutekeleza kwa ufanisi jukumu hili” alisema
na kuongeza kuwa:
“Ni
muhimu kwa watumishi wa Tume katika utendaji kazi wao kuepuka vitendo
vya ukiukwaji wa maadili kama vile rushwa, upendeleo na au ubaguzi wa
aina yoyote katika sehemu ya kazi”
Mbali
na hayo, Mhe. Jaji Kaijage aliipongeza Tume kufanikisha uchaguzi mdogo
uliofanyika mwezi Januari mwaka huu katika jimbo la Dimani na kata 20 za
Tanzania Bara kwa kuufanya kuwa wa amani na utulivu pamoja na
changamoto mbalimbali zilizoukabili uchaguzi huo.
Mbali
na kutoa maelekezo hayo Mgeni rasmi huyo wa ufunguzi wa kikao cha
Baraza la wafanyakazi wa NEC, alitoa wito kwa wajumbe wa kikao hicho na
watumishi wote wa Tume kuitafsiri kaulimbiu ya Hapa Kazi Tu kwa vitendo
na kuzingatia matakwa ya Katiba, Sheria, Kanuni na miongozo mbalimbali.
Alieleza
matumaini yake juu ya umoja na ushirikiano uliopo Tume kwamba
vitaimarika na kuwa taasisi hiyo itatekeleza majukumu yake kwa ufanisi,
kujenga nguvu na mshikamano wa pamoja kwa wafanyakazi wote.
Katika
kikao hicho cha siku mbili mada mbalimbali ziliwasilishwa ikiwemo
Mapitio ya mwaka 2016/2017 na Makisio ya Bajeti ya mwaka 2017/2018,
Wajibu wa Mtumishi, Dawa za Kulevya na Athari zake kwa jamii na Namna ya
Kupambana na Ugonjwa wa Ukimwi.
“Ninaomba
mjadili mada hizo kwa kina na busara mkitambua kuwa matokeo ya
majadiliano yenu ni kwa ajili ya maslahi ya Tume na taifa kwa ujumla”
alisema Mhe. Jaji Kaijage na kufafanua kuwa:
“Kwa
kuwa kipind hiki ni cha bajeti nashauri na kusisitiza mjadili kwa kina
vipaumbele vya bajeti vya taasisi ili viwe ni msingi wa kuiwezesha Tume
kuwa na ubunifu na uthubutu wa kuibua mawazo mapya yatakayoiwezesha
kupiga hatua zaidi na utendaji kazi bora wa kila siku”
Aliwakumbusha
wajumbe kuwa mabaraza ya wafanyakazi yameundwa kwa mujibu wa Waraka wa
Rais Namba 1 wa mwaka 1970 na moja ya madhumuni ya kuanzishwa kwake ni
kuongeza ufanisi na tija kazini.
Aliongeza
kuwa kanuni za Kudumu za Utumishi wa Umma toleo namba 3 la mwaka 2009,
limefafanua kuwa lengo ni kutoa uwanja wazi wa majadiliano kati ya
watumihsi na waajiri katika kutoa maamuzi katika masuala ya ajira.
Hivyo
aliwawaomba wajumbe wa baraza la wafanyakazi la Tume watumie fursa ya
kikao hicho kuwawakilisha wafanyakazi wenzao vizuri kwani vikao vya
baraza ni sehemu muhimu ya kujadili namna ya kuboresha mazingira ya kazi
na kutimiza malengo yake.
“Uzoefu
unaonesha kuwa mabaraza ya wafanyakazi yanapotumika vizuri hali ya
maelewa na utulivu sehemu za kazi huongezeka na hivyo kuongeza tija
kazini” alisema.
Akimkaribisha
mgeni rasmi, Mwenyekiti wa Baraza hilo ambaye ni Mkurugenzi wa Uchaguzi
wa NEC Bw. Kailima Ramadhani, mbali na kuwambusha wajumbe lengo la
kuanzishwa mabaraza ya wafanyakazi, alisema baraza pia lina wajibu wa
kutoa maagizo mbalimbali kwa ajili ya kuboresha na kutekeleza malengo ya
taasisi.
Aliongeza
kuwa baraza pia ni eneo ambalo mwajiri anapaswa kutoa ufafanua kwenye
maeneo ambayo watumishi watahitaji kupata ufafanuzi hasa kuwasilisha
mapendekezo ya mwelekeo wa Bajeti ya Taasisi kabla haijawasilishwa
kwenye Kamati ya Bunge.
Wakati akimshukuru mgeni rasmi kwa ufunguzi, Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya (Tughe) Taifa Bw. Heri Mkunda alimueleza mgeni rasmi jinsi anavyoridhishwa na jinsi baraza la wafanyakazi linavyopewa umuhimu na Tume.
Bw.
Mkunda pia alimpongeza Mhe. Jaji Kaijage kwa kuteuliwa kuwa Mwenyekiti
wa Tume na kwamba Tughe Taifa wana imani naye atatimiza vyema ujenzi wa
demokrasia nchini na kuahidi kutoa ushirikiano wa kutosha kwake ili
kutimiza lengo hilo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)