Sunday, March 19, 2017

HIZI NDIO SABABU ZA KUPANDA KWA BEI YA NYANYA TANZANIA






Gharama ya bidhaa za vyakula imezidi kupanda kadri siku zinavyozidi kusonga huku bei ya nyaya ikionekana kupanda zaidi. Wafanyabiashara wa zao hilo katika masoko tofauti tofauti hapa Dar es salaam wamesema kuwa wakati uliopita nyaya zilikuwa nyingi sana ila kwa sasa zimekuwa adimu.

Miongoni mwa sababu hasa zilizofanya kupotea kwa zao hilo ni uwepo wa mvua nyingi zilizoathiri usafirishaji pamoja uzalishaji mwingi uliofanyika msimu uliopita hivyo watu wengi wakaambulia hasara.

Sanduku moja ilikuwa ni Tsh. 30,000 mpaka 28,000, kilo moja Tsh. 1,500 na nusu kilo Tsh. 800 ila kwa sasa bei ya sanduku moja ni Tsh. 75,000 mpaka 60,000, sadolini moja Tsh. 14,000, kilo moja Tsh. 3,000 na nusu kilo Tsh. 1,500.

Wateja wa bidhaa hizi za vyakula wamesema kuwa siyo nyaya peke yake zilizopanda bei ila ni kwa vitu vingine pia ikiwemo maharage na unga wa mahindi.

Mtaalamu wa uchumu, Dkt. Hosiana Lunogelo amesema kuwa tatizo ni kushindwa kupishanisha uzalishaji wa mazao ya msimu. Hasa yale yanayoharibika kwa muda mfupi kama nyanya. Vinginevyo yanatakiwa yasindikwe na bado hatujawekeza vya kutosha katika usindikaji.

0 Responses to “HIZI NDIO SABABU ZA KUPANDA KWA BEI YA NYANYA TANZANIA”

Post a Comment

More to Read