Sunday, March 19, 2017
MUUNGANO WA MADAKTARI WA KENYA (KMPDU) WAWAKATAA MADAKTARI WA TANZANIA
Do you like this story?
Umoja
wa Madaktari, Wauguzi na Wataalamu wa Meno nchini Kenya ‘Kenya Medical
Practitioners, Pharmacists and Dentists’ Union’ (KMPDU) umepinga vikali hatua
ya Serikali ya Kenya kuleta madaktari kutoka Tanzania wakati Kenya ina
madaktari wengi ambao hawaajiriwa.
Kupitia
kwa Katibu Mkuu wa KMPDU, Ouma Oluga umepinga hatua hiyo na kudai kuwa Serikali
ya Kenya haijawa makini katika kushughulika na tatizo la upungufu wa madaktari
nchini humo.
Akizungumza
na mtandao wa The Star wa nchini Kenya siku ya Jumamosi, Oluga alisema hata
hivyo watawakaribisha madaktari kutoka Tanzania na kuwaunganisha katika umoja
huo na kwamba watapaswa kupitia mitihani itakayoandaliwa na bodi ya wauguzi.
Amesema
mitihani hiyo itachukua sio chini ya miezi mitatu labda kama tu hitaji hilo
halitaangaliwa.
“Kenya
ina zaidi ya madaktari 1,400 ambao wanasubiria ajira. Itakuwa gharama kubwa na
dalili ya kushindwa kutumia fedha za umma vizuri kwa kuwa na madaktari 500 wa
kitanzania kwa gharama ya Shilingi 20,000 kwa siku,” amesema.
Oluga
amesema kuwa Kenya inapaswa kupitia upya utaratibu wake wa Rasilimali Watu kwa
mujibu wa miongozo ya Afya kama ambavyo KMPDU imekuwa ikihitaji hapo kabla.
“Hatuwezi
kuwa tunafanyia majaribio maisha ya wakenya katika hali inayoonesha kutowajali
wananchi,” ameongeza.
Mapema
jana Rais Magufuli alikubali na kuridhia ombi la Serikali ya Kenya na kuahidi
kutuma madaktari 500 kusaidia kukabiliana na tatizo la upungufu wa madaktari
nchini humo kufuatia mgomo wa madaktari ulioisha hivi karibuni baada ya kudumu
kwa siku 100.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ MUUNGANO WA MADAKTARI WA KENYA (KMPDU) WAWAKATAA MADAKTARI WA TANZANIA”
Post a Comment