Wednesday, March 22, 2017
KABULI LA YESU LAFUNGULIWA UPYA JERUSALEM
Do you like this story?
Timu ya wanasayansi na wakarabati wamekamilisha kazi katika eneo
linalodaiwa kuwa ni kaburi la Yesu Kristo katika mji wa zamani wa Jerusalem, na
itafunguliwa wazi kwa umma siku ya Jumatano.
Kundi hilo limefanya kazi hiyo kwa muda wa miezi tisa kwenye
Kanisa la Mtakatifu Sepulchere na walilenga katika sehemu ndogo ya juu ya
kaburi, inayojulikana kama ‘Edicule’.
Waumini wengi wa dini ya kikristo wanaamini kuwa mwili wa Yesu
ulizikwa katika eneo lililokuja kuwa Kanisa la Mtakatifu Sepulchre.
Mzozo kati ya madhehebu matatu ambayo kwa pamoja husimamia kanisa
hilo likiwemo Kanisa la Kiothodoksi la Ugiriki, Kanisa la Kiarmenia na Kanisa
Katoliki la Kirumi ulichelewesha ukarabati huo kwa miongo mingi.
Kazi ilianza mwaka jana baada ya mamlaka ya Israel, ambayo imekuwa
ikiiongoza Mashariki ya Jerusalem tokea ilipoiteka katika vita ya Mashariki ya
Kati mnamo mwaka 1967, kusema kuwa kanisa hilo siyo salama kwa kuwa chumba
hicho kilikuwa kimekuwa dhaifu sana kiufundi.
Aidha, kilikuwa kimechakaa na kubadilika rangi na kuwa karibu
rangi nyeusi kutokana na masizi ya mishu
maa mingi ambayo huwashwa eneo hilo.
Antonia Moropoulou, aliyesimamia ukarabati huo, amesema chumba
hicho sasa kimepata tena rangi yake asili inayokaribia hudhurungi.
Vyombo vya habari vimeripoti kuwa kila dhehebu limechangia mradi
huo. Mfalme Abdullah wa Jordan nae alitoa mchango wake binafsi, kazi yote
iligharimu takribani dola za kimarekani bilioni 3.3
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ KABULI LA YESU LAFUNGULIWA UPYA JERUSALEM”
Post a Comment