Thursday, March 9, 2017
PIGANO LA PACQUIA NA AMIR KHAN LAFUTILIWA MBALI
Do you like this story?
Bondia wa Uingereza
Amir Khan hatopigana na bingwa wa uzani wa Welterweight Manny Pacquiao
mwezi ujao kulingana na promota Bob Arum
Mabondia hao wawili
walikuwa wametangaza pigano hilo kufanyika mnamo mwezi Aprili 28 katika
mtandao wa Twitter mwisho wa mwezi Februari huku UAE ikitajwa kuwa eneo
la pigano hilo.
Lakini Arum ameambia ESPN: Pigano hilo limefutiliwa mbali.
''Ninazungumzia kuhusu pendekezo jingine lakini sio Khan.Khan hatakuwa mpinzani wa Manny''.
Pigano
hilo la mwezi Aprili lilipangwa baada ya mashabiki wa Paqcuiao katika
mtandao wa Twitter kumpigia kura Khan kuwa mpinzani ambaye wangependelea
bondia huyo mwenye umri wa miaka 38 kupigana naye.
Khan mwenye
umri wa miaka 30 aliyeshinda medali ya fedha katika uzani wa Lightweight
katika michezo ya Olimpiki ya 2004, alimshinda Kell Brook, raia wa
Australia Jeff Horn na Mmarekani Terence Crawford kwa asilimia 48 ya
kura hizo zilizofanywa na Pacquiao.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “PIGANO LA PACQUIA NA AMIR KHAN LAFUTILIWA MBALI”
Post a Comment