Thursday, March 9, 2017

ZAIDI YA WATU 30 WAMEUAWA


  Makomandoo wa Afghanstan walidondoshwa kwenye paa la hospitali ya Sardar Daud

Zaidi ya watu 30 wameuawa, kulinga na maafisa, lakini baadhi ya ripoti zinasema kuwa idadi ya vifo huenda ikawa kubwa zaidi.
Makamanda wa Afhanstan tayari wametua kwenye baa la hospitali hiyo ya Sardar Daud na sasa wanapigana na wanamgambo.
Kundi la Islamic State(IS) limedai kuhisika na shambulio hilo.
Taleban wamekanusha kuhusika, kulingana na ripoti ya vyombo nchini humo.

Rais Ashraf Ghani amesema kuwa shambulio hilo kwenye hospitali ya Sardar Daud hospital yenye uwezo wa kuwalaza wagonjwa 400 ni "uvunjaji wa maadili yote ya binadamu".
" Katika dini zote, hospitali inachukuliwa kama mahala penye kinga na kuishambulia ni kuishambulia Afghanstan nzima ," alisema .
IS wamekuwa wakiendesha harakati zao nchini Afghanistan tangu mwaka 2015 na tayari wamekwisha tekeleza mashambulio kadhaa nchini humo.
Ilidai kuwajibika na ulipuaji wa mashambulio ya kujitoa muhanga katika mahakama kuu ya mjini Kabul mwezi uliopita ambapo watu 22 waliuawa.
Kundi linalojiita jimbo la Khorasan, ambalo linaunganisha mataifa ya Afghanistan na Pakistan, hivi karibuni limeanza harakati zake katika mataifa yote mawili.
 
Moshi ukifuka kwenye paa la hospitali wakati wa shambulio 
Wapiganaji wa Taleban pia wamekuwa wakiendesha mashambulio yaliyowauwa watu 16 mjini Kabul katika mashambulio yaliyokuwa ya kujitolea muhanga.
Shambulio lilianza saa tatu unusu kwa saa za Aghanstan wakati mwanamgambo alipojilipua katika lango moja la upande wa kusini mwa hospitali- ambayo iko karibu na ubalozi wa Marekani- halafu washambuliaji wengine watatu wa wakaingia ndani ya mazingira ya hospitali hiyo.
Wakaingia katika ghorofa la pili na la tatu huku wakiwa na silaha ndogo pamoja na gurunati na kuanza kufyatua risasi.
 
Police wamefunga eneo la tukio 
Mhudumu mmoja wa hospitali ambaye aliweza kutoka nje alimuona mshambuliaji "akiwa amevalia koti jeupe amesikilia bunduki aina ya Kalashnikov na kumfyatulia risasi yeyote, wakiwemo walinzi, wagonjwa na madaktari". Mhudumu mmoja aliandika kwenye ukurasa wa Facebook: "washambuliaji wako ndaniya hospitali. Tuombeeni."
Mmoja wa washambuliaji ameuawa na wengine walikuwa wamejificha chini ya ngazi, alisema msemaji wa wizara ya ulinzi. Askari mmoja pia ameuawa na wengine watatu wamejeruhiwa na wagonjwa wanaokolewa kupitia milango ya kutokea ya dharura.
Takriban watu watatu wamekufa na wengine zaidi 60 wamejeruhiwa, wengi wao wakiwa ni wahudumu wa hospitali, amesema waziri wa afya na pia vyombo vya habari.

0 Responses to “ZAIDI YA WATU 30 WAMEUAWA”

Post a Comment

More to Read