Thursday, March 23, 2017
POLISI ZANZIBAR IMEWAKAMATA WASAMBAZAJI 200 WA DAWA ZA KULEVYA
Do you like this story?
Jeshi
la Polisi Tanzania, kanda ya Zanzibar imewakamata wasambazaji 200 wa
Madawa ya kulevya wakiwemo wasambaji maarufu wapatao 32 waoendelea
kuhojiwa na jeshi hilo.
Akizungumza
na Waandishi wa habari Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai
Zanzibar Ramadhani Ng`anzi amesema ukatwaji huo umekuja baada ya
upelelezi uliofanywa na jeshi la polisi kwa makundi matatu ya watu
wakiwemo wafanyabiashara na kubahatika kuwakamata wasambazaji hao.
Hata
hivyo amesema katika operesheni hiyo pia madawa ya aina mbalimbali
yamekamatwa ikiwemo Heroin na Cocain Grams 3450.32,madawa mengine ni ya
vidonge valium 493, Bhangi 203 na Mirungi kg46 pamoja na gari moja na
pikipiki tatu ambazo zilikuwa zinatumika kusambazia biashara hiyo.
Aidha
amesema opereshen hiyo imeleta faida kubwa kwa jamii na jeshi la
Polisi kutokana na kupungua kwa vigenge vya madawa ya kulevya na kutoa
wito kwa wananchi kuendelea kutoa ushirikiano ili wahusika waweze
kuchukuliwa hatua za kisheria.
Jumla
ya shilingi millioni nne laki tatu na ishirini elfu zimekamatwa katika
operesheni hiyo na kesi 87 zimefunguliwa tangu kuanza kwa operesheni
hiyo february mwaka huu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)