Wednesday, March 22, 2017
WABUNGE WA CUF WAKAMATWA KWA MADAI YA MAUAJI
Do you like this story?
WAKATI
Baraza Kuu la Uongozi la Chama cha Wananchi (CUF), likitoa maazimio
yake ikiwemo kubariki kuvuliwa kufurushwa kwa kuvuliwa uanachama vigogo
wake, wabunge wawili wa chama hicho wanashikiliwa na Jeshi la Polisi
mkoani Dodoma kwa tuhuma za kutishia kumuua mbunge mwenzao.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Lazarto Mambosasa, alisema kuwa wabunge hao
wamehojiwa kutokana na tuhuma za kudaiwa kumtishia kumuua Mbunge wa
Kaliua, Magdalena Sakaya (CUF).
Viongozi
hao wa CUF wamekuwa na mvutano ndani ya chama kwa muda mrefu sasa na
kupelekea kuzaliwa kwa makundi mawili likiwemo linalomuunga mkono
Mwenyekiti anayetambuliwa na Msajili wa Vyama, Profesa Ibrahim Lipumba
na lile linalomuunga mkono Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif
Sharif Hamad.
Kamanda
Mambosasa, alisema baada ya mahojiano na wabunge hao jeshi hilo
liliwaachia huru ili waweze kuendelea na majukumu yao na kutakiwa kufika
polisi pale watakapohitajika.
“Ni
kweli tumewahoji sababu kubwa ni kumtishia kumuua Mbunge mwenzao Sakaya
ila tumewahoji tu na kuwaachia waendelee na shughuli zao,’’ alisema
Akizungumzia
Sakata hilo, nje ya Kituo cha Polisi, Katibu wa wabunge wa CUF, Juma
Kombo Hamad, ambaye pia ni Mbunge wa Wingwi, alisema wabunge hao
walikamatwa kutokana na taarifa zilizotolewa na Sakaya kuhusu kutishiwa
maisha ambapo alisema hayo ni masuala la kisiasa.
“Haya ni mambo ya kisiasa tu yakataa vizuri na maisha yataendelea,’’ alisema Juma
Jana
Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa CUF, Julius Mtatiro alitangaza
maazimio la kikao cha Baraza Kuu laUongozi lililoketi Visiwani Zanzibar
ambapo kikao hicho kilibariki kuvuliwa uanachama kwa vigogo wake saba
ambao, ni Mohamed Habibu Mnyaa, Haroub Shamis, Mussa Haji
Kombo, Khalifa Suleiman Khalifa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “WABUNGE WA CUF WAKAMATWA KWA MADAI YA MAUAJI”
Post a Comment