Wednesday, April 12, 2017
Mahakama yamfutia Gwajima kesi ya lugha ya matusi dhidi ya Kardinali Pengo
Do you like this story?
Mahakama yamfutia Gwajima kesi ya lugha ya matusi dhidi ya Kardinali Pengo
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, leo
imefuta kesi iliyokuwa inamkabili Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima,
Josephat Gwajima ya kumtolea lugha chafu Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki
Jimbo Kuu la Dar es Saalam, Kardinali Polycarp Pengo.
Uamuzi wa kufutwa kesi hiyo umetolewa na Hakimu wa mahakama hiyo,
Cyprian Mkeha baada ya upande wa mashtaka kupitia kwaA Wakili wa Serikali
Mwandamizi, Joseph Maugo, kuomba kesi hiyo iahirishwe kwa kuwa hawakuwa
na shahidi wa pili. Upande wa Jamhuri umeleta shahidi mmoja pekee ndani
ya kipindi cha miezi 14.
Hakimu Mkeha alitumia kifungu cha 225 cha Sheria ya Mwenendo wa
Mashauri ya Jinai (CPA) kufuta kesi dhidi ya kiongozi huyo wa dini.
Katika kesi ya msingi, Askofu Gwajima ambaye alipandishwa kizimbani
kwa mara ya kwanza Aprili 17 mwaka 2015 anadaiwa kutoa lugha ya matusi
dhidi ya Kardinali Pengo kati ya Machi 16 na 25 mwaka 2015, akiwa katika
viwanja vya Tanganyika Packers vilivyoko Kawe jijini Dar es Salaam.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “Mahakama yamfutia Gwajima kesi ya lugha ya matusi dhidi ya Kardinali Pengo”
Post a Comment