Wednesday, April 12, 2017

Daily Mail kumlipa Melania Trump kwa kumchafulia jina


Gazeti la Uingereza la Daily Mail limekubali kumlipa mke wa rais wa Marekanai Melania Trump, kutokana na uharibifu uliosababishwa na taarifa iliyochapishwa na gazeti hilo.
Gazeti hilo lilikuwa limeandika kuwa Melania Trump wakati mmoja alifaya kazi kama kahaba.
Taarifa hiyo ilichapjshwa wakati wa kampeni nchini Marekani.
Bi Trump alikubali msamaha kutoka kwa gazeti hilo kwenye mahakama mjini London.
Alipeleka kesi mahakamani mwezi Februari, akitaka kulipwa dola milioni 150.
Pesa ambazo Melania Trump alikubali kulipwa hazikufichuliwa.
Hata hivyo ripoti kutoka kwa shirika la Reuters zilisema kwa makubaliano hayo yalikuwa ya chini ya dola milioni 3.
Alisajiliwa na shirika moja la mitindo akiwa bado msichana na kuanza kusafiri kote Ulaya na Marekani na kushiriki katika warsha kubwa.
Alikutana na Donald Trump mwaka 1998, akiwa na umri wa miaka 28 kwenye sherehe wakati wa wiki ya mitindo mjini New York.
Walifunga ndoa miaka saba baadaye.

0 Responses to “Daily Mail kumlipa Melania Trump kwa kumchafulia jina”

Post a Comment

More to Read