Wednesday, April 12, 2017

Makubwa: Maiti Yatozwa faini Huko Manyara


Kiongozi wa kimila katika Kijiji cha Endagulda ameamriwa akamatwe baada ya kuitoza faini maiti.
Mkuu wa Wilaya ya Mbulu mkoani Manyara, Chelestino Mofuga aliagiza kukamatwa na kufunguliwa mashtaka kiongozi huyo.A
Mofuga ametoa agizo hilo juzi kijijini hapo baada ya baadhi ya wananchi kulalamika kuwa, mzee wa kimila, Joseph Daniel aliagiza Gadii asizikwe hadi faini hiyo itakapolipwa.
Awali, kiongozi huyo wa kijiji aliagiza kulipwa faini ya ng’ombe mmoja kutoka kwenye zizi la marehemu Boay Gadii (42) kabla ya maziko yake ikielezwa kuwa alitengwa na jamii.

0 Responses to “Makubwa: Maiti Yatozwa faini Huko Manyara”

Post a Comment

More to Read