Thursday, April 13, 2017
Mchakato wa Kuziba Pengo la Sophia Simba Bungeni Waiva
Do you like this story?
Tume
ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeutaarifu Umma juu ya kuendelea na
taratibu za kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Mbunge wa Viti
maalumu(CCM) Sophia Simba aliyefukuzwa uanachama wa Chama cha
Mapindizi (CCM) Machi 11, mwaka huu.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi Jaji(R) Semistocles Kaijage imeeleza kuwa Spika wa Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amemjulisha Mwenyekiti wa Tume kuwa
kufuatia Mbunge huyo kufukuzwa uanachama wa CCM hivyo kiti cha Mbunge
huyo kiko wazi.
Alisema
kuwa Ibara ya 67(1) (b) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya
mwaka 1977 inaeleza kuwa ili mtu ateuliwe au achaguliwe katika nafasi
ya ubunge ni lazima awe mwanachama aliyependekezwa na Chama chake husika
cha siasa.
“Kwa
kuwa ndugu Sophia Mnyambi Simba amefukuzwa uanachama wa Chama
kilichomdhamini, Ibara ya 67(2)(e) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania inaelekeza kuwa mbunge huyo amepoteza sifa za kuteuliwa au
kugombea Ubunge” alisema Jaji(R) Semistocles Kaijage.
Aliendelea
kwa kusema kuwa kutokana na kuwepo kwa nafasi hiyo taratibu za kujaza
nafasi hiyo zinaendelea kwa kuzingatia kifungu cha sheria 86(8) cha
Sheria ya Uchaguzi Sura ya 343.
Kifungu
hicho kinasema, orodha ya majina wanawake wagombea waliopendekezwa na
tume kwa mujibu wa Ibara 78(4) ya Katiba na kila chama cha siasa kwa
uchaguzi mkuu, kwa kuzingatia Ibara 76(3) ya Katiba, itakuwa orodha
sawa na ile itakayotumiwa na tume kwa madhumuni ya kujaza nafasi yoyote
iliyowazi katika ofisi ya mbunge wa viti maalum vya wanawake wakati wa
kipindi kizima cha uwahi wa Bunge.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)