Wednesday, April 12, 2017

MKUU WA MKOA ASIMAMISHA UJENZI WA SOKO LA UHINDINI BAADA YA KUBAINI BAADHI YA WAHANGA KUTOTENDEWA HAKI


Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amosi makalla akizungumza na wafanya biashara wa Soko la Uhindini ambalo liliungua.(Picha na David Nyembe wa Fahari News Mbeya)

Wafanyabiashara wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Mkoa.(Picha na David Nyembe wa Fahari News Mbeya)

Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Bw William Ntinika akitoa neno la utangulizi kwa fanyabiashara
.(Picha na David Nyembe wa Fahari News Mbeya)

Wafanyabiashara wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Mkoa

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya Bw Zackaria Nachoa akimpa maelezo Mkuu wa Mkoa juu ya Soko hilo(.(Picha na David Nyembe wa Fahari News Mbeya)


Mkuu wa Idara ya Ujenzi Halmashauri ya Jiji la Mbeya Bw Lawrean Sanya akiongea na wafanyabiashara juu ya utaratibu wa Ujenzi katika Soko hilo la Uwindini.(Picha na David Nyembe wa Fahari News Mbeya)
Wafanyabiashara wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Mkoa

Mmoja wa Wafanyabiashara wahanga akitoa kero yake kwa Mkuu wa mkoa .(Picha na David Nyembe wa Fahari News Mbeya)

Baadhi ya Majengo ambayo Mkuu wa Mkoa amepiga Marufuku ujenzi kuendelea kutokana na kuona wanaojenga sio waanga wa Soko hilo la Uhindini.(Picha na David Nyembe wa Fahari News Mbeya)


Mmoja wa Wafanyabiashara wahanga akitoa kero yake kwa Mkuu wa mkoa

Baadhi ya Majengo ambayo Mkuu wa Mkoa amepiga Marufuku ujenzi kuendelea kutokana na kuona wanaojenga sio waanga wa Soko hilo la Uhindini.(Picha na David Nyembe wa Fahari News Mbeya)




Amesema uamuzi wa kuwarejesha  wahanga ni kutokana na Ramani ya Mipango miji na Amesema alikataa mpango wa jiji wa kuligeuza eneo Hilo kuwa eneo la Kuegesha magari.

Hata hivyo amesimamisha ujenzi wa soko Baada ya kuwabaini baadhi ya  majina yametoka kwa viongozi wa kisiasa na hivyo kuwanyima haki WAHANGA halisi wa soko lililoungua miaka 7 iliyopita na sasa wanarejeshwa.
 
 Amesema hakuna ujenzi utakaoendelea mpaka mambo Muhimu yatakapozingatiwa ikiwemo
Mosi, uhakiki wa wahanga  ufanywe upya , kila mtu aonyeshe alikuwa anafanya eneo gani kwenye hilo soko wakati soko la Uhindini halijaungua na WAHANGA wenyewe wanajuana na watathibitisha.

Pili, majina yawekwe wazi  kila mmoja aone na kama kuna majina wanatilia Shaka waseme na orodha hiyo ipelekwe Kamati maalumu ya soko kisha kuthibitishwa na jiji
Tatu, Ramani ya  soko ipitiwe na wadau( WAHANGA) na wataalaam na iridhiwe
NNE, Kila MHANGA ( mpangaji) awe na mkataba unaoeleza Gharamaya  kujenga chumba na marejesho gharama katika kodi
TANO, maduka au vibanda vijengwe kwa viwango vitakavyokubalika vya mfano na ujenzi na viwango utasimamiwa na jiji.

Hata hivyo amesisitiza kuwa uamuzi wa kuwarejesha  wafanyabiashara hao umezingatia ramani ya Mipango miji inaonyesha eneo hilo ni soko na hakukubaliana na hoja ya jiji kutaka kugeuza eneo hilo kuwa Maegesho ya magari
Ameuagiza uongozi wa jiji kukamilisha mchakato huo ndani ya  Siku 21( wiki Tatu).

 Wananchi wamepongeza sana uamuzi huu kwani bila Mkuu wa Mkoa kuingilia Baadhi ya wahanga wangenyimwa haki na kupatiwa watu wengine

0 Responses to “MKUU WA MKOA ASIMAMISHA UJENZI WA SOKO LA UHINDINI BAADA YA KUBAINI BAADHI YA WAHANGA KUTOTENDEWA HAKI”

Post a Comment

More to Read