Sunday, April 16, 2017
MJUE MWIGIZAJI WA FILAMU YA YESU AMBAYE BAADHI YA WATU HUDHANI KWAMBA NI YESU.
Do you like this story?
Brian Deacon akiigiza kama Yesu ndani ya filamu ya JESUS. |
Ikiwa leo ni Ijumaa kuu,siku ambayo wakristo ulimwenguni wanakumbuka
mateso ya mkombozi wa ulimwengu Yesu Kristo aliyekuja duniani takribani
miaka 2000 iliyopita.Gospel kitaa imeamua basi kuwaletea historia ya mtu
ambaye ameigiza filamu ya Yesu inayofahamika kwa jina la ”JESUS” ambayo
iliigizwa mnamo mwaka 1979 huko nchini Israel, GK imeamua kufanya hivi
baada ya kuona ni kwa jinsi gani filamu hiyo imekuwa ikigusa maisha ya
watu wengi kiasi kwamba baadhi ya watu wanasahau kwamba mtu aliyemo
kwenye filamu hiyo ni mwigizaji tu na siyo Yesu.hata yeye amekiri kwamba
wakati wa uigizaji alikuwa akisuluhisha mambo yaliyokuwa yakijitokeza
yeye na waigizaji wenzake baada ya wao kusahau kwamba yeye si Yesu bali
anaigiza tu. KARIBU.
Brian Deacon ndani ya filamu ya ”JESUS” |
Brian Deacon ndio jina lake mwigizaji huyo ambaye ni mwingereza
aliyezaliwa mnamo tarehe 13/02/1949 huko Oxford nchini Uingereza akiwa
ni mtoto wa pili katika familia yao baba yake akiwa fundi makenika na
mama yake akiwa ni nesi ndoa yake ya kwanza na Rula Lenska ilivunjika
ambapo alizaa na mkewe huyo binti yao aitwaye Lara Deacon,ndoa yake ya
pili alioana na mwanamama Natalie Bloch mnamo mwaka 1998 mpaka sasa wapo
kwenye ndoa hiyo.
Aliigiza filamu ya Yesu ambayo pia ilimfanya aokoke mara baada ya
kuitazama akiwa na miaka 30,baada ya kupita kwenye mchujo mkali wa
waigizaji zaidi ya elfu moja ambao walifanyiwa mahojiano huku 260
wakijaribishwa kuigiza(screen test)kuona kwamba wanafaa akiwa ni
mwingereza pekee kati ya waigizaji Waisrael walioingia kwenye usaili huo
akiwa chini ya kampuni iitwayo New shakespears ambako alikuwa akifanya
sanaa za majukwaani na uigizaji.
Brian Deacon miaka iliyofuatia baada ya kuigiza kama Yesu. |
Amesema kabla ya kuchaguliwa mtihani wake wa kwanza ulikuwa kutoka kwa
wakala wake aliyemvunja moyo kwakumweleza hadhani kama yeye(Brian)atafaa
kwenye kumwigiza Yesu,lakini anasema alifanikiwa,baada ya hapo akawa na
wakati mgumu kutoka kwa watu ambao kila mmoja alikuwa anajaribu
kumweleza jinsi anavyotakiwa kuigiza,sauti yake na mambo mengine,ingawa
yeye alisema nitatumia sauti yangu na maelezo kutoka kwa
muongozaji.Amesema wiki tatu kabla hawajaanza kurekodi filamu hiyo
alisoma kitabu cha Luka mtakatifu zaidi ya mara 20 kwakuwa filamu hiyo
imenukuliwa kutoka kitabu hicho ambapo Brian amesema kusoma kwake
kulimpa nguvu sana na moyo wa kuigiza filamu hiyo na kuweza kumfahamu
vyema Yesu kuwa ni mtu wa aina gani.
watu wakiangalia filamu ya Yesu ambayo bwana Brian Deacon ni mwigizaji mkuu. |
Katika miezi saba waliyochukua kuigiza filamu hiyo Brian
amesema,walikuwa wanaigiza kwa masaa mengi kuanzia saa kumi za alfajiri
mpaka mwisho wa siku kiasi kwamba wakati mwingine aliwaambia wenzake
kwamba wamsaidie kwani amechoka sana hajui kwamba angeweza kuigiza kwa
siku hiyo lakini anasema alikuwa anashangazwa na nguvu za ajabu
alizokuwa akizipata na kuendelea kuigiza ingawa wakati huo nasema
alikuwa mkristo jina wa kanisa katoliki,alikuwa anauwalakini kuhusu
mafundisho na huduma ya Yesu kwa ujumla,siku moja wakati anaigiza
alikuwa anawaombea watu mara mwanamke mmoja alishika mkono wake kumbe
alikuwa na mapepo alimuombea na mapepo yalimtoka mwanamama huyo.
Siku nyingine waliokuwa wakiigiza kama wanafunzi wa Yesu wapatao 12
wakiwa ndani ya basi walikuwa wamepanga kugoma kutokana na malipo
waliyokuwa wakipata cha ajabu Brian anasema director alikuja kumuomba
yeye (Brian) azungumze nao warejee kazini akashangaa akamwambia mimi sio
Yesu ni Brian Deacon, akaamua kuzungumza nao, baada ya masaa 36
walikubali kurudi kuendelea na kazi.
Amesema mtihani mwingine ni siku alipokuwa hotelini Tel Aviv ghorofa ya
18 usiku mara kukawa na moto hotelini hapo baada ya mwingereza mmoja
aliyekuwa akivuta sigara kusahau kuizima hivyo kusababisha moto,lakini
anasema bahati nzuri hakuna aliyejeruhiwa ila walifanya kazi siku
inayofuatia muda mrefu bila muongozaji kujali kwamba hawakulala vyema
usiku.
watumishi wa Mungu wakiwa njiani kwenda kuonyesha filamu ya Yesu katika uinjilisti huko Kongo. |
Amesema siku hiyo mmoja wa waigizaji anayeitwa Tom Panella alianzisha
mada kwa kusema moto uliokuwa umetokea ni hila za shetani,na kusababisha
mjadala wa muda mrefu ni vipi shetani anahusishwa kwenye swala hilo
lakini jibu likawa,shetani hataki filamu hiyo irekodiwe ndio maana
analeta hila zake.haikuwa kazi rahisi kurekodi filamu hiyo na pia si
ujuzi wa kufurahia,baada ya kumaliza kurekodi kwa takribani miezi 18
ilianza kuonyeshwa kwa baadhi ya watu na ndipo hata yeye kwa mara ya
kwanza akaona ni kwa jinsi filamu hiyo ilivyonanguvu,ukweli na kugusa
mioyo ya watu.
Baada ya filamu hiyo Briana anasema alirudi kuigiza majukwaani na kwenye
runinga, ambapo kwa miaka zaidi ya 30 sasa tangu kutoka filamu ya Yesu
tayari imetazamwa na watu zaidi ya bilioni tatu katika nchi 133 (kwa
takwimu za mwaka 2001), zaidi ya watu milioni 117 waliamua kubadilisha
maisha yao na kumpokea Yesu,filamu hiyo ambayo ilitengenezwa chini ya
Campus Crusade for crusade ambao kwasasa wanaitwa Life Ministry pia
nchini Tanzania wapo chini ya mkurugenzi Dismas Shekhalage.ambapo tayari
imetafsiriwa katika lugha zaidi 500 huku nyingine zaidi ya 200 zikiwa
njiani kutafsiriwa.
Brian anawaambia watu kwamba yeye ni mwigizaji tu na sio Yesu kama watu
wengine na kuwataka watu hao kujua hivyo ambapo anasema ameendelea
kupata barua mbalimbali za kumpongeza na kumshukuru kwa kazi nzuri
aliyofanya kwenye filamu hiyo,ambapo kwa upande wake anasema anayo
nakala ya filamu hiyo kwenye maktaba yake nyumbani kwao Uingereza,ambapo
kwa takribani miaka 20 filamu hiyo imekuwa ikitazamwa duniani kote na
kubadilisha maisha ya watu.
Kati ya filamu alizowahi kushiriki ni pamoja na A zed & Two Noughts
ya mwaka 1985, The Feathered Serpent ya mwaka 1976-1978 na Tamthilia
iitwayo Lillie iliyoigizwa mwaka 1978 akitumia jina la Frank Miles.
Huyo ndiye Brian Deacon mwigizaji mkuu wa filamu ya ”JESUS”iliyoigizwa
mwaka 1979 huko nchini Israel. Habari kwa msaada wa mtandao.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MJUE MWIGIZAJI WA FILAMU YA YESU AMBAYE BAADHI YA WATU HUDHANI KWAMBA NI YESU.”
Post a Comment