Friday, April 7, 2017

Mwanamuziki wa Ubelgiji atua nchini kutengeneza wimbo na Harmorapa


pic+hamorapa
Mwanamuziki Kriticos wa nchini Ubelgiji leo amewasili nchini kwa lengo la kufanya wimbo pamoja na msanii chipukizi wa Tanzania anayekuja kwa kasi sana, ajulikanae kama Harmorapa.
Mara baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere mchana leo, mwanamuziki Kriticos ambaye anaimba miondoko ya kufokafoka ‘rap’, amesema kuwa anavutiwa na aina ya uimbaji ya Harmorapa na ndiyo sababu kuu iliyomfanya aje hapa nchini ili kufanya naye kazi.
Kwa upande wake Harmorapa anayetamba na kibao chake cha Kiboko ya Mabishoo alichomshirikisha Juma nature, amesema kuwa ujio huo kwake ni heshima kubwa na utamfanya atambulike zaidi kimataifa.
Pia amewataka mashabiki wake kukaa mlo wa kula. Ngoma hiyo itatengenezwa na kurekodiwa na mtayarishaji wa muziki, P-Funk majani.

0 Responses to “Mwanamuziki wa Ubelgiji atua nchini kutengeneza wimbo na Harmorapa”

Post a Comment

More to Read