Friday, April 7, 2017

Wanandoa washinda BETTING kwa mara ya tatu


lo
Wanandoa Barbara na Douglas Fink kutoka nchini Canada, wamejikuta wenye bahati mara baada ya kushinda mchezo wa bahati nasibu kwa mara ya tatu. Wanandoa hao ambao umri wao umeanza kuwa wa makamo sasa, wameeleza kuwa wamekuwa wakishiriki michezo mbalimbali ya bahati nasibu na kwa mara ya tau wameweza kushinda kitita kikubwa kuliko vingine vyote walivyowahi kushinda hapo awali.
Walieleza kuwa mwaka wa 1989 ulikuwa ndiyo mara ya kwanza kwao kushinda mchezo wa bahati nasibu ambapo walipata dola za kimarekani 128,000 sawa na TZS milioni 285. Mwaka wa 2010 walishinda dola 100,000 sawa na TZS milioni 223.
Ushindi wao wa hivi punde wa dola za Marekani milioni 6.1 ambao ni sawa na TZS bilioni 13.6, ndio ushindi mkubwa zaidi kwao.
Wanandoa hao kutoka Edmonton, Alberta wanasema watatumia pesa hizo kukimu mahitaji ya watoto wao na wajukuu pia.
“Familia ndio muhimu, Tunataka kuhakikisha kuwa watoto wetu wa kike na watoto wao wako sawa.” Barbara aliwaeleza waratibu wa michezo hiyo.
Douglas anasema pia watatumia kiasi cha pesa hizo kusafiri maeneo mbali mbali na nyingine kununulia nyumba mpya.
“Barbara anataka nyumba mpya, na ataipata.” Alieleza shirika la michezo ya bahati nasibu la ‘Western Canada Lottery’
Ni wao tu na mtu mwingine mmoja ambao waliweza kukisia kikamilifu nambari zote sita zinazohitajika ili kushinda mchezo huu. Barbara alisema yeye ndiye aliyegundua kuwa wao ni washindi, mumewe akiwa kazini katika mji mwingine.

0 Responses to “Wanandoa washinda BETTING kwa mara ya tatu”

Post a Comment

More to Read