Friday, April 7, 2017

YAJUE HAYA KABLA YA KUAMUA KUJICHORA TATTOO (Share na Wenzako)


1.Hazifutiki milele, swali linakuja je, miaka kadhaa ijayo utaendelea kukipenda kitu ambacho umekipenda leo nakukichora? Mfano, unadhani unakipenda Ulichokuwaukikipenda kufanya miaka 10 iliyopita? Kazi


2.Ili kuweza kuzoea tattoo unashauriwa kuchora tattoo ya muda mfupi kabla hujaamua kuchora tattoo ile itakayobaki milele.


3.Huwezi kuchangia damu katika baadhi ya mataifa. Ni vema kujua sheria za nchi yako kwanza kabla ya kufanya uamuzi huo.



4.Usikurupuke kuchora tattoo, kuwa na wazo la aina ya tattoo ya kitu unachokihitaji sio tu kwa kuwa uliiona kwa mtu Fulani.
5.Huharibu muonekano wako katika jamii kwani kuna badhi ya sehemu unaweza usishirikishwe kwa kuonekana hufai katika jamii ile (hasa jamii za Kifrika)

6.Kuchora tattoo ni gharama, kabla ya kujichora tattoo lazima ujipange kwanza ili upate kitu unacho kihitaji kwa gharama sahihi na kuepuka tattoo ya ubora wa chini na kutokuwa na muonekano unaoutaka.

7.Ni hatari labda tu uchorwe na mtu mwenye uwezo mkubwa wa kuchora kwani kuna miili ina ‘aleji’ na wino utumikao kuchora tattoo. Yaani eneo ulilochora mchoro wa tattoo, linaweza kudhurika kwa namna mbalimbali.

8.Tattoo itakufanya ukose baadhi ya kazi kwani kuna baadhi ya sehemu tattoo huonekana kama ni ukosefu wa nidhamu. Mfano Jeshini, baadhi ya Mashirika ya Kidini nk!

9.Usidhani unajua sana undani kuhusu tattoo  kwa kuwa tu uliona watu kwenye tv  wakiwa na tattoo na wewe ukatamani kuwa nayo, Hakikisha una elimu ya kutosha kuhusu tattoo unayotaka kuichora ndipo ufanye maamuzi.


10.Kuwa makini katika uchaguzi wa mahali sahihi katika mwili wako ambako unahitaji uchore tattoo hiyo.

0 Responses to “YAJUE HAYA KABLA YA KUAMUA KUJICHORA TATTOO (Share na Wenzako) ”

Post a Comment

More to Read