Thursday, April 3, 2014
HATI YA MUUNGANO MVURUGANO.
Do you like this story?
Dodoma. Utata umezidi
kuibuka katika bunge maalumu la katiba
kutokana na kutopatikana kwa hati ya muugano wa Tanganyika na Zanzibar na ile ya sheria ya baraza la mapinduzi ya kuridhia mkataba wa muungano.
Utata huo umebainika
katika kamati kadhaa siku moja tangu
wajumbe wa bunge hilo waanze
kujadili sura ya kwanza nay a sita ya rasimu ya katiba zinazohusu jamhuri ya muungano wa Tanzania na muundo wake.
Jana kamati namba 2
ilimwalika spika mstaafu wa bunge la
muungano pius umsekwa kutoa ufafanuzi
kuhusu hati hizo lakini uhalali wa saini zake uliibua malumbano makali.
Msekwa aliitwa kutokana na kwamba ndiye
aliyekuwa katibu wa bunge la Tanganyika
wakati huo.
Mwenyekiti wa kamati hiyo
shamsi vuai nahodha alithibitisha
kutokea utata huo na kwamba walilazimika
kumuita msekwa ililiwapa
ufafanuzi wa masula kadhaa.
Nahodha alisema kwa
maelezo ya msekwa inaonekana hati ya
muugano pia umoja wa mataifa kwani kabla ya muungano Tanganyika ilikuw na kiti
chake UN na jamhuri ya watu wa zanzibari hali kadhalika.
Nahodha alisema baada ya
UN kuomba uthibitisho wa muugano
ndipo walipelekewa hati hiyo na kwamba haijawahi kurejeshwa.
Kauli hiyo ya nahoda
inapingana nakauli ya katibu wa bunge la
katiba yahya hamis hamad ambaye jana
alisema hati hiyo ipo dare s salaam na
ni moja tu hivyo siyo rahisi kuipeleka bungeni Dodoma.
Ile hati ya muungano ipo
dare s salaam lakini tunahofia kuileta
maana inaweza kupotea kwani ni
moja tu sasa ambacho tutakifanya inaweza kutolewa nakala na kuthibitishwa na mawakili na ijaja nakala
Dodoma iwapo wajumbe wanahitaji alisema hamad.
Katika hatua nyingine
sheria namba 22 ya 1964 ya baraza la
mapinduzi Zanzibar kuridhia muungano nayo haijulikani ilipo.
Baadhi ya wajumbe katika
kamati namba 2 walidokeza kuwa walipohoji kuhusu sheria hiyo walisomewa kitabu
cha aliyewahi kuwa mwnasheria wa
Zanzibar abdul jumbe ana kuambiwa kwamba picha za ukumbusho zipo.
Nahodha ambaye aliwahi
kuwa waziri kiongozi wa Zanzibar alikiri kuwa hatayeye hajawahi kuona sheria hiyo.
Kwa bunge la Tanganyika
ushahidi tumeletewa hapa kuwa waliridhia april 25 1964 walosaini ni Julius
nyerere katibu wa bunge hilo na pius
msekwa na aliyekuwa spika adam sapi
mkwawa lakini kwa Zanzibar haupo alisema
na kuongeza.
“mimi nilikuwa mtendaji
mkuu wa SMZ nilipaswa kujua lakini nisingeweza
tu kuanza kutafuta sheria , sheria ambazo zimetungwa Zanzibar ni nyingi
kwani ingeniwia kazi ngumu sana kuipata
hati hii kwani msimamizi wake ni ofisi ya katibu mkuu wa baraza la mapinduzi ,
ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali au
ofisi ya rais”
Alsiema mwanasheria mkuu
wa Zanzibar Othman masoud Othman pia alisema hajawai kuiona sheria hiyo.
Utata wa saini.
Kuhusu utata wa saini za
nyerere na mskekwa kwenye hati hizo nahodha alisema yeye siyo mtaalamu wa maandishi kubaini kuwa hati
hizo na saini zake ni halali au la.
\
Hata hivyo alisema msekwa
alikiri kwenye kamati hiyo kuwa saini iliyopo
kwenye hati ya makubaliano ya
muungano niyake.
Utata wa saini za
msekwa uliibuliwa na baadhi ya wajumbe
ambao walihoji tofauti bainan saini
iliyopo kwenye sheria hati ya muugano na
saini zake katika nyaraka nyingine rasmi.
Wajumbe waliomba msekwa
waliongwzwa na godbless lema pia waliitia shama matumizi ya kompyuta katika sheria hizo zilizoandikwa mwaka 1964
Mwaka 1964 hakukuwa na
kompyuta lakini hapa tuanona sheria
zimebandikwa kwa komputa na hata sehemu
ya saini ya msekwa na nyerere kuna herufi
zimeandikwa kwa kompyuta alinukuliwa
lema.
Katika maelezo yake msekwa
licha ya kikiri upungunfu
aliwakumbusha wajumbe kuw siku ya
kusainiwa hati hizo picha zilipigwa na
zipo hadi sasa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “HATI YA MUUNGANO MVURUGANO.”
Post a Comment