Thursday, April 3, 2014

KINANA: TUJILAUMU KWA MAREKEBISHO YA KATIBA Z’BAR.




Nkasi. Katibu mkuu wa CCM ablulrahma kinana amesema  hoja zilizoshawishi  marekebisho ya kumi ya katiba ya Zanzibar  hazikuwa na mashiko ya kujenga  utaifa , badala yake zilikuwa na sababu za kuleta mpasuko usiokuwa na tija kwa watanzania.

Akizungumza  kinana amesema marekebisho hayo yaliyoitambua  Zanzibar  kuwa nchi ni makosa  ambayo pande zote mbili za muungano zinatakiwa kuyajutia  kwa kukosa umakini nakuhisi kuwa ongezeko la mambo ni kuzikandamiza .

Kwa mujibu wa marekebisho hayo , Zanzibar  ilitambuliwa kuwa nchi na kumpokonya  mamlaka ya rais wa jamhuri wa muungano wa Tanzania katika ugawaji  wa mkoa na wilaya kisiwani humo na kumpa mamlaka rais wa Zanzibar .

Alifafanua kuwa baada ya kuvunjika kwa jumuiya ya afrika mashariki mwaka 1977 sehemu zote mbili za muungano  hazikuona ukweli ni upi  mpaka kufikia muundo  ulioleta mgogoro wa kikatiba mpaka sasa.

Alisema sababu nyingine ya kufanya marekebisho hayo ni pamoja na msukumo wa kisiasa  kutoka kwa nvyama vya upinzani .

Kinana alionya kuhusu mgawanyiko  akisema ni vyema tukakumbuka  athari za uzanzibari  na uzanzibara  zilizoelezwa  na mwaklimu Julius nyerere.

Azidi kumpinga warioba.

Kinana aliendelea kupingana na mapendekezo  ya muundo wa serikali tatu ya tue ya mabadiliko  ya katiba iliyoongozwa na jaji warioba akisisitiza kuwa waziri huyo mkuu  wa zamani anatakiwa kutoa ufafanuzi kuhusu hoja zilizofichika.

Hata hivyo jaji warioba alipohojiwa na gazeti hili kuhusu madai hayo alisema nisingependa  kuzungumzia tena suala hilo kwa sababu nilishaeleza kila kitu bungeni.

0 Responses to “KINANA: TUJILAUMU KWA MAREKEBISHO YA KATIBA Z’BAR.”

Post a Comment

More to Read