Thursday, April 3, 2014
MWALIMU AMCHAPA MWANAFUNZI HADI AKAFA...!!!!!
Do you like this story?
Wazazi
katika kaunti ya Kirinyaga mkoa wa Kati nchini Kenya wameandamana kwa hasira
baada ya mwalimu kumchapa mtoto mmoja wa shule ya msingi hadi akafariki.
Mtoto
huyo inaarifiwa alichapwa kichwani na mwalimu na kuzirai. Alifariki alipokuwa
anapelekwa hospitalini.
Wazazi
hao waliandamana kwa amani wakitaka hatua kali kuchukuliwa dhidi ya mwalimu
huyo.
Hata
hivyo polisi waliweza kumkamata mwalimu huyo na kumpeleka kituoni huku
uchunguzi ukianza kufanywa.
Mtoto
huyo alikuwa katika darasa la saba katika shule ya kibinafsi ya Roka
Preparatory.
Inaarifiwa
alizirai baada ya mwalimu kumchapa kwenye kisogo.
Wazazi
hao waliokuwa wanalalamikia kile wanachosema ni wanafunzi kuadhibiwa vikali kwa
makosa madogomadogo walitaka mwalimu huyo achukuliwa hatua kali kwa kitendo
hicho cha kumchapa mwanafunzi ambacho kimeharamishwa katika shule zote nchini
Kenya.
Wengi
wa wazazi wenye watoto wao katika shule hiyo wameahidi kuwahamishia shule
nyingine.
Kenya
iliharamisha kitendo cha kuwachapa wanafunzi wa shule karibu miaka kumi
iliyopita. Ilikuwa baada ya visa vya walimu kuwaadhibu vikali wanafunzi na
kuwajeruhi kukithiri.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ MWALIMU AMCHAPA MWANAFUNZI HADI AKAFA...!!!!! ”
Post a Comment